Cristiano Ronaldo ndiye mfungaji bora | Michezo | DW | 14.10.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Cristiano Ronaldo ndiye mfungaji bora

Mchezaji nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo ametunukiwa kiatu cha Dhahabu kwa Ufungaji Bora barani Ulaya na kuweka rekodi kwa kutwaa taji hilo kwa mara ya nne

Katika msimu wa 2014/15, Ronaldo alifunga mabao 48 kwenye ligi kuu ya Uhispania La Liga na kutwaa Njumu ya Dhahabu kwa mara 3 akiwa na miamba Real Madrid

Msimu wa 2007/08 akiwa na Manchester United alitwaa tena kiatu hicho baada ya kuwa mfungaji bora. Hii ni mara ya kwanza katika Historia ya Miaka 47 ya Tuzo hii ya Njumu ya Dhahabu kwa Mfungaji Bora wa Ligi za Ulaya kuichukua mara 4.

Ronaldo, ameifungia Real Madrid jumla ya mabao 323, na kufikia rekodi ya mabao mengi iliyokua imewekwa na mchezaji wa zamani wa timu hiyo Raúl González aliyefungia timu hiyo mabao 323.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Abdulrahman