1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COVID-19 yauwa karibu watu elfu 70

Sudi Mnette
6 Aprili 2020

Mataifa ambayo yameshambuliwa vibaya na mripuko wa corona barani Ulaya yameonesha kupigia hatua katika makabiliano ya vita dhidi ya virusi hivyo pamoja na kwamba ugonjwa wake umemlaza hospitali Waziri Mkuu wa Uingereza.

https://p.dw.com/p/3aUwy
Vatikan Papst Franziskus Palmsonntag
Picha: Reuters/Vatican Media

Virusi vya corona vimeiathiri kila pembe ya dunia ambapo vimegharimu maisha ya watu karibu elfu 70 na kusababisha maambukizi yanayopindukia watu milioni 1.2. Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza alitoa hutoba yake na kuwataka waingereza, pamoja na mataifa yaliyo katika Jumuiya ya Madola kusalia kuwa na mshikamano na umoja katika kipindi hiki kigumu.

Kumekuwa na habari za matumaini katika maeneo tete ya maambukizi hayo kama Italia, kuwa na ripoti ya chini ya idadi ya watu wanaokufa katika kipindi cha wiki mbili. Uhispania kadhalika viwango vimeshuka kwa siku tatu mfululizo wakati Ufaransa nayo ikiwa na rekodi ndogo ya vifo kwa juma zima. Afisa mmoja wa afya nchini Italia Silvio Burusaferro alisikia akisema hatua itakayofuta inaweza kuwa kupunguka vikwazo vya kufanyika kwa shughuli kadhaa za kawaida nchini humo ambavyo vimedumu kwa mwezi mzima.

Spanien Leganes | Coronavirus | Patient Notaufnahme
Mgonjwa wa COVID-19 wa UfaransaPicha: Reuters/S. Vera

Wagonjwa mahututi wa Uhispania hawaongozeki

Huko Uhispania, muuguzi  Ampar Lero alinukuliwa na vyombo vya habari akisema "Hali imekuwa madhubuti" Idadi ya wagonjwa ambao wapo katika wodi za watu mahututi haiongezeki, na wameanza kuwaruhusu wachache miongoni mwa wagonjwa hao.

Mzigo mkubwa unaelekea Marekani ambapo watu waliokufa kwa sasa inakaribia watu 10,000 na serikali ya taifa hilo limeonya kwamba hatari inalinyemelea zaidi.

Jimbo la New York ambalo limeathiriwa zaidi, kwa sasa lina vifo 4,159, ikiwa kiwangpo kikubwa ililinganishwa na siku moja kabla ambapo vilikuwa vifo 3,565. Kanisa kubwa la ibada la Roma, ibada ambayo kwa kawaida inayoongozwa na kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis, jana Jumapili vilikuwa vitupu kabisa, hiyo ikiwa ishara kuepusha maambukizi zaidi ya virusi.

Huko Barani Asia, Waziri Mkuu Shinzo Abe anatarajiwa kutangaza hali ya dharura, ingawa sheria haimpi nguvu ya kuwalazimisha watu kusalia majumbani. Uturuki matumani yanapungua kwa kuwa idadi ya maambukizi ya virusi vya corona imeongezeka na kupindukia watu 27,000. Idadi ya waliokufa imefikia 73 kwa usiku wa kuamkia leo na kufanya jumla ya waliokufa kufikia 574.

Nchini India jumla ya watu 109 wamkufa kutoka na ugonjwa waCOVID 19, miongoni mwa vifo hivyo 32 vimetokea ndani masaa 24 ikumumuisha maambukizi mapya 693.