CORD Kenya kufanya maandamano | Matukio ya Afrika | DW | 27.05.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

CORD Kenya kufanya maandamano

Muungano wa upinzani nchini Kenya CORD unaoongozwa na Raila Amolo Odinga unapanga kuanzisha harakati kubwa za umma kudai mabadiliko nchini humo.

Kenia Wahlen Raila Odinga

Wafuasi wa muungano wa CORD wakiwa na kiongozi wao Raila Odinga

Harakati hizo zilizopewa jina Okoa Kenya zinakuja katika wakati ambapo nchi hiyo imezongwa na ukosefu wa Usalama pamoja na kitendawili cha kashfa nzito ya mabilioni ya fedha ya Anglo Leasing. Katika kipindi cha Kinagaubaga Saumu Mwasimba amezungumza na kaimu mwenyekiti wa CORD Prof Anyang Nyon'go. Kusikiliza mahojiano hayo bonyeza alama ya kusikilizia masikioni hapo chini.

Mwandishi: Saumu Mwasimba
Mhariri: Sudi Mnette

Sauti na Vidio Kuhusu Mada