1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COPENHAGEN:Wanne wakamatwa kwa kutaka kufanya ugaidi

4 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBSe

Idara ya ujasusi ya Denmark imesema kuwa imewakamata watu wanane baada ya kuwashuku kuwa walikuwa na mikakati ya kufanya shamulizi la kigaidi.

Mkuu wa Idara hiyo ya Ujasusi ya Denmark amesema kuwa washukiwa hao wenye umri kati ya miaka 19 na 28 ni wanamgambo wa kiislam wenye imani kali ambao wanamaingiliano na kundi la kigaidi la Al Qaida.

Watu hao walikamatwa katika msako wa jana usiku jijini Kopenhagen, ikiwa ni mara ya tatu kwa polisi kufanya operesheni hiyo katika kipindi cha miaka miwili, ambapo watu kadhaa walikamatwa wakihusishwa na masuala ya ugaidi.