1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Clinton amwidhinisha Obama

6 Septemba 2012

Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton ametoa hotuba ya kina kumpigia debe Rais Barack Obama aweze kurejea ikulu kwa mhula wa pili katika uchaguzi wa rais mwezi Novemba.

https://p.dw.com/p/164ET
President Barack Obama joins former President Bill Clinton (R) onstage after Clinton nominated Obama for re-election during the second session of the Democratic National Convention in Charlotte, North Carolina, September 5, 2012. REUTERS/Jason Reed (UNITED STATES - Tags: POLITICS ELECTIONS) // Eingestellt von wa
Barack Obama / Bill Clinton / USA / US-Demokraten / CharlottePicha: Reuters

Hotuba hiyo ya Clinton ilichukua dakika 49 muda ambao ndio mwingi zaidi kuliko wazungumzaji wengine katika mkutano mkuu wa Chama cha Democratic unaoendelea mjini Charlotte, jimbo la North Carolina.

Katika hotuba iliyokuwa na maelezo ya kina ya kumwidhinisha Obama, Clinton alizungumzia hoja ambayo imeikumba kampeni ya Obama, kwamba wapiga kura wanakabiliwa na chaguo baina ya sera za chama cha Democratic zenye mafanikio au sera za chama cha Republican ambazo huwafaidisha matajiri kwa gharama ya watu wengine. Lakini Bill Clinton hakukomea hapo.

Michelle Obama aliufungua mkutano huo mkuu wa chama cha Democratic akimpigia debe mumewe apewe muda zaidi
Michelle Obama aliufungua mkutano huo mkuu wa chama cha Democratic akimpigia debe mumewe apewe muda zaidiPicha: Reuters

Huku akionekana kutofuata hotuba yake ya mandishi , Clinton alifafanua masuala muhimu ambayo hayajazungumziwa katika kongamano hilo. Aliusifu mpango wa kichocheo cha uchumi ambao Obama aliweka mnamo wa 2009, upanuzi wake wa msaada wa masomo ya vyuo na juhudi zake za kuboresha nishati mbadala.

Rekodi ya Obama yasifiwa

Alifafanua jinsi sheria ya Obama ya huduma za afya ilivyowanufaisha wamarekani wa kawaida, na akaonya kuwa pendkezo la Warepublican kupunguza matumizi ya huduma za afya kunaweza kuwaathiri watu masikini katika jamii. Alihoji kuwa warepublican huenda wakaendeleza matatizo ya kifedha ya nchi hiyo na kuwazuia watu zaidi dhidi ya kupiga kura.

Clinton ameuambia umati kuwa "Wakati tukipiga kura katika uchaguzi huu, tutakuwa tunaamua ni nchi ipi tunataka kuishi. Kama unataka mshindi achukue kila kitu , basi utakuwa katika jamii ya aina yako, unaweza kumunga mkono mgombea wa chama cha republican. Lakini kama unataka nchi ya kugawana fursa na wajibu, tutakuwa katika jamii moja, unafaa kumpigia kura Barack Obama na Joe Biden"

Hasimu wa Obama wa chama cha Republican Mitt Romney, hajaeleza waziwazi mambo anayopendekeza katika kampeni yake, huku akifafanua tu kuhusu mapendekezo yake kupunguza gharama za matumizi na kurahisisha kodi.

Barack Obama tayari yuko Charlotte, North Carolina
Barack Obama tayari yuko Charlotte, North CarolinaPicha: Getty Images

Clinton alihoji kuwa wakati maelezo yakwia bado hayajulikani, sera za Romney huenda zikiaongeza deni la kitaifa, kuwakekea mzigo wa kadoi wananchi wa kitengo cha wastani, au kuathiri mipango kama vile lishe bora kwa watoto na uchukuzi.

wengi wa wazungumzaji katika mkutano huo wameyalenga masuala kadhaa kama vile haki za uzazi na msamaha kwa watoto wa wahamiaji haramu, ambayo yanaonekana kuwa masuala muhimu yanayoiongezea uzito kambi ya Democratic.

Clinton kwa upande wake aliwalenga watu wengi, kwa kufafanua mafanikio ya Obama kwa ujumla pamoja na mapendekezo ya Romney. Alilenga kuzinyakua kura za wapiga kura huru ambao badi hawana uhakika kama wakimpa Obama muda wa miaka mingine minne madarakani, wataona mabadiliko mazuri.

Rais Obama amewasili katika kongmanao hilo na anatarajiwa kuuhutubia umati wa takribani watu 74,000 katika uwanja wa michezo baadae leo .

Mwandishi: Bruce Amani/Reuters

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman