1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUingereza

City na United wako tayari kwa kombe la FA

2 Juni 2023

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema wachezaji Kevin De Bruyne na Jack Grealish wako katika kiwango kizuri kushiriki azma yao ya kushinda makombe matatu katika fainali ya Kombe la FA dhidi ya United.

https://p.dw.com/p/4S8Fc
Chelsea Women v Manchester United Women - The Women's FA Cup - Wembley Stadium
Picha: Gary Oakley/Zumapress/picture alliance

De Bruyne, Grealish, Ruben Dias na Manuel Akanji wote walikosa mechi ya mwisho ya City ya Ligi Kuu msimu huu huko Brentford wiki iliyopita na sasa Guardiola amesema wachezaji hao wanne wamerejea mazoezini na wanatarajiwa kuhusika katika fainali ya kwanza inayozikutanisha timu mbili za Manchester katika Kombe la FA huko Wembley.

 Soma pia: Ten Hag: Carabao ni motisha wa makombe zaidi

Guardiola pia amethibitisha kwamba mlinda lango Stefan Ortega atajumuishwa katika kikosi cha kwanza dhidi ya United badala ya kipa Ederson.

Ortega, ambaye alianza mechi mbili kati ya tatu zilizopita za ligi, hajaruhusu bao lolote katika Kombe la FA msimu huu.

Ni hatua ya kijasiri kutoka kwa Guardiola, ambaye timu yake imebakisha mechi mbili kabla ya kuwa klabu ya pili ya Uingereza -- baada ya United mwaka 1999 kushinda Ligi ya Premia, Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa katika msimu mmoja.

Ingawa City ilisonga mbele kwa taji kwa ushindi mara 12 mfululizo wa ligi na kumaliza pointi 14 mbele ya United, Guardiola hana nia ya kudharau timu ya Erik ten Hag.

Je itakuwa rahisi?

Manchester City v Arsenal/Kevin de Bruyne und Erling Haaland
Picha: Simon Stacpoole/Offside Sports Photography/IMAGO

United iliishinda City 2-1 mwezi Januari, na kulipiza kisasi cha kupoteza kwao 6-3 mapema kwenye kampeni, na pia ilimaliza ukame wao wa miaka sita wa kutwaa taji hilo kwa kunyakua Kombe la Ligi mwezi Februari.

Ikiwa City wataifunga United, wanaweza kukamilisha hatua tatu katika fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Inter Milan mjini Istanbul mnamo Juni 10. Lakini Guardiola amewataka wachezaji wake kutotazamia azma yao ya kutwaa taji la kwanza la Ligi ya Mabingwa.

Tukifikiria mataji, la pili au la tatu, ni lazima tuchambue uimara wa mpinzani wetu, tuangalie udhaifu alionao,” alisema Guardiola.

Kocha wa Manchester United Erik ten Hag anahofia kuwa mshambuliaji  wake Antony "hawezi" kupona jeraha kwa wakati ili kushiriki katika fainali FA baada ya kutolewa nje kwa machela katika kipindi cha kwanza cha ushindi wa wiki iliyopita wa Ligi ya Premia dhidi ya Chelsea.

 soma pia: Sevilla yashinda Kombe la Ligi ya Ulaya baada ya kuifunga Roma kupitia penalti

Lakini licha ya changamoto za udhabiti wa mwili inayoisumbua timu yake, Ten Hag anasalia na imani kuwa United wana nguvu ya kuwashinda wapinzani wao City.