1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China yatoa mwito wa kukomeshwa vita vya Ukraine

24 Februari 2023

China imetoa mwito wa kusitishwa kwa mapigano kati ya Ukraine na Urusi na kuanzishwa kwa mazungumzo ya amani katika pendekezo la vipengele 12 la kusitisha mapigano yaliyoanza mwaka mmoja uliopita.

https://p.dw.com/p/4NvVy
Deutschland | Ukrainische Flaggen am Reichstag in Berlin zum 1. Jahrestag der russischen Angriffs auf die Ukraine
Picha: Fabrizio Bensch/REUTERS

China ambayo inadai kutoegemea upande wowote katika mzozo huo, lakini ikisema ina "urafiki usio na kikomo" na Urusi imekataa kukosoa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, imezishutumu nchi za Magharibi kwa kuchochea mzozo kwa kuipatia Ukraine silaha za kujihami.

Wakati hayo yakiendelea mkuu wa kundi la wapiganaji mamluki la Urusi Wagner, Yevgeny Prigozhin amesema leo Ijumaa kwamba, wapiganaji wake walikiteka kijiji karibu na mji wa Bakhmut mashariki mwa Ukraine, eneo ambalo mapigano makali yameshuhudiwa kwa miezi kadhaa.