1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chelsea hatimaye yanunuliwa

9 Mei 2022

Chelsea hatimaye wamepata mnunuzi wa klabu yao baada ya kuwekwa mnadani na mkwasi kutoka Urusi Roman Abramovich.

https://p.dw.com/p/4B2zf
FC Chelsea
Picha: Nick Potts/PA/empics/picture alliance

Mmiliki mpya wa miamba hao wa London Magharibi sasa ni Todd Bohly aliyekuwa uwanjani juzi akiishuhudia timu yake kutoka sare ya mabao mawili na Wolverhampton Wanderers uwanjani Stamford Bridge.

Ni habari njema kwa klabu hiyo hatimaye kupata mnunuzi kwa kuwa chini ya Abramovich ilikuwa imewekewa vikwazo na serikali ya Uingereza na hakuna biashara zozote ilizokuwa inaweza kuendesha hata kuuza tiketi za kila siku kwa mashabiki.

FC Chelsea
Mmilki wa zamani wa Chelsea Roman AbramovichPicha: Marc Atkins/Offside/picture alliance

Ila kocha Thomas Tuchel anasema hakuna lolote litakalobadilika kwa sasa licha ya mmilki mpya kupatikana.

"Hakuna mengi yatakayotubadilikia kwasababu vikwazo vingalipo na msimu utaendelea tu kwa hiyobado tunatarajia kwamba kutakuwa na matokeo chanya na hali inayotuzunguka itatuliwe. Kwa sasa inaonekana kana kwamba imetatuliwa ila bado, hata hakuna haja ya kuifikiria. Tuna mambo yetu mengi ya kufikiria na kuyaboresha kwasababu tunapitia kipindi kigumu kwa sasa," alisema Tuchel.