Champions League | NRS-Import | DW | 30.09.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

NRS-Import

Champions League

Bayern Munich yateremka uwanjani leo dhidi ya Olympique Lyon

default

Kocha Klinsmann
Kinyanganyiro cha kombe la klabu bingwa barani Ulaya-champions League kikirudi leo na kesho uwanjani,mabingwa Manchester United wana miadi leo na Aalborg ya huko Denmark wakati mabingwa wa Ujerumani-Bayern Munich changamoto ya jioni hii na Olympique Lyon ya Ufaransa, huenda ikaamua hatima ya kocha wao mpya Jurgen klinsmann,kwani Munich imeanza vibaya sana msimu huu wa Bundesliga na iko sasa nafasi ya 9 ya ngazi ya Ligi.


Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich watataumai leo kusahau kushindwa kwao mara mbili mfululizo katika Bundesliga hivi majuzi -pigo la karibuni ni la jumamosi walipozabwa bao 1:0 na Hannover.Munich imeanza vibaya kabisa msimu huu wa Ligi tangu kupita miaka 31,wakiwa wameshinda mechi 2 kati ya 6 na sasa kichwa cha kocha wao mpya Jurgen klinsmann kinatakiwa kufyekwa na mashabiki. Klinsmann aliepata sifa nyingi alipoingoza Ujerumani katika kombe lililopita la dunia,anaelewa lazima Munich itambe leo mbele ya Olympic Lyon.


Katika kinyanganyiro hiki,Munich haikuanza vibaya.Iliilaza Steua Bukarest ya Rumania bao 1:0 na ushindi mwengine leo katika champions league, utamukoa Klinsmann na timu yake.

Mabingwa watetezi wa kombe hili-Manchester united wanaanza kutetea taji lao huko copenhagen,denmark ambako leo wakitamba na jogoo lao Cristiano Ronaldo,watapania kuondoka na pointi zote 3.Hii ni muhimu kwao baada ya kumudu sare tu nyumbani duriu iliopita walipopambana na Villarreal ya Spian.

Villa inacheza leo nyumbani dhidi ya Celtic ya Scotland.


Timu za Uingereza zikitazamiwa tena kutia fora msimu huu,Arsenal, ina miadi leo na mabingwa wa zamani wa kombe hili FC Porto ya ureno.Arsenal lakini ilikumbwa na msukosuko mwishoni mwa wiki ilipozabwa bao 1:0 tena nyumbani na chipukizi Hull City.

Real Madrid,mabingwa mara kadhaa wa kombe hili la Ulaya wamefunga safari leo hadi St.Petersburg,Russia kwa miadi na Zenit St.Petersburg.

Mabingwa hawa wa Spian wanacheza leo bila wachezaji wake stadi wa kiungo kama Fernando Gago,Wesley Sneider wa Holland .Hatahivyo, Real ina matumaini mazuri kufuatia ushindi wao wa dakika ya mwisho mwishoni mwa wiki walipotamba nyumbani mbele ya Real Betis.Real ilishinda kwa mabao 2:1 shukurani kwa bao la Van Nistelrooy.

Real lakini wako kileleni pamoja na Juventus ya Itali katika kundi lao. Juventus inaitembelea leo Bate na yatumai kushinda tena.


Chelsea ya Uingereza iliopokonywa kombe Mei mwaka huu na mahasimu wao wa nyumbani Manchester United wameanza uzuri nyumbani katika premier-league.Wanalenga leo ushindi wao wapili katika kombe hili wakiumana jioni hii na Cluj-Napoca ya Rumania.

Hatahivyo, Chelsea itabidi kucheza bila ya Deco,Carvalho na Mghana Essien.

Mabingwa wa Itali Inter Milan walilazwa kwa mara ya kwanza msimu huu kwa bao la mwishoni mwa wiki la Ronaldinho wa AC milan.Lakini, mbele ya wajerumani Werder Bremen wanatumai kutamba.

FC Barcelona kesho ina miadi pia na Shakhtar Donetsk wakati mabingwa mara 5 wa Ulaya FC Liverpool wanatamnba nyumbani dhidi ya waholanzi PSV Eindhoven.
 • Tarehe 30.09.2008
 • Mwandishi Ali, Ramadhan
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/FRbH
 • Tarehe 30.09.2008
 • Mwandishi Ali, Ramadhan
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/FRbH
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com