Champions League | Michezo | DW | 15.09.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Champions League

Kombe la klabu bingwa barani Ulaya laanza msimu mpya.

Kombe la klabu bingwa barani Ulaya-champions League linaanza leo huku klabu 2 za Spian-FC Barcelona na Atletico Madrid zikianza katika hali isioridhisha.Barcelona ina miadi na Sporting Lisbon. Karlheinz Rummenigge, anaazamia kwa mara nyengine tena klabu za Uingereza kutamba kama msimu uliopita.

Rummenigge alielezea hofu kwamba klabu za Bundesliga kama vile Schalke inayoicheza leo na Nicosia, hazitafua dafu.

►◄

FC Barcelona ikicheza leo nyumbani ikiikaribisha Sporting Lisbon kwa mapambano ya kundi C inajikuta imeanza vibaya sana msimu mpya wa La Liga-Ligi ya Spian hali ambayo haijawahi kujikuta tangu 1973.Barcelona imenyakua pointi 1 tu hadi sasa huku Espanyol ikiongoza orodha ya Ligi ya nyumbani.

Thierry Henry,Rafa Marquez na Martin Caceres wote hawakucheza mwishoni mwa wiki pale Barcelona ilipłomudu suluhu tu nyumbani ya bao 1:1 na Racing Santander.

Katika changamoto za kundi D Atletico Madrid-klabu nyengine ya Spian,mabingwa wa Ulaya wana kibarua hata kigumu zaidi kuliko Barcelona:

Wana miadi na PSV Eindhoven ya Holland baada ya kuzabwa nyumbani mabao 2:1 na Valladolid.

Liverpool inaumana leo na Olympic Marseille nchini Ufaransa.Klabu nyengine ya Premier League uwanjani leo itakua Chelsea inayopambana na timu nyengine ya Ufaransa -Girondins Bordeaux. Chelsea inabidi kucheza bila stadi wake wa kiungo Michael Ballack.Kocha Felipe Scolari adai huenda akamchezesha japo kidogo Ballack.

Werder Bremen ya Ujerumani inayocheza kwa mara ya 5 mfululizo katika champions League, inaikabili Famagusta ya Cyprus inayoshiriki kwa mara ya kwanza katika kombe hili.

Mkurugenzi wa klabu bingwa ya Ujerumani-Bayern munich,Karlheinz Rummenigge ,amesema jana anazitazamia klabu za Uingereza kwa mara nyengine tena kutia fora msimu huu na kutamba katika champions League.Ameelezea pia wasi wasi kwamba klabu za Ujerumani zitazidi kurudi nyuma.Rummenigge amema kwamba Premier League iko mbele hivi sasa ya Ligi nyengine za Ulaya.dhidi ya