Champions League uwanjani tena leo: | Michezo | DW | 21.02.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Champions League uwanjani tena leo:

Mabingwa wa Ulaya FC Barcelona bila ya stadi samuel Eto'0 inaingia uwanjani leo kupambana na FC Liverpool ya Uingereza.Real madrid jana iliitoa Bayern munich kwa mabao 3:2.

Changamoto Real na B.munich

Changamoto Real na B.munich

Baada ya jana duru ya kwanza ya champions League kumalizika kwa ushuindi wa mabao 3:2 wa Real Madrid ya Spain dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani,leo ni zamu ya mabingwa wa Ulaya FC Barcelona kuteremka uwanjani lakini bila ya mshambulizi wao kutoka Kamerun ,Samuel Eto’o.Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani,Bernd Schüster,amejitolea kuwa kocha mpya wa Bayern Munich.

Mabiongwa wa Ulaya FC Barcelona wanachuana hivi punde na FC Liverpool ya Uingereza .Simba wa nyika-mkamerun Samuel Eto’0 aliekorofishana na kocha Frank Rijkaard na mwenzake Ronaldinho,ameachwa leo nje ya chaki ya uwanja.E to’o ni mchezaji bora wa mwaka x 3 wa Afrika na ni mtiaji mabao mengi kwa Barcelona alieibuka mtiaji mabao mengi msimu uliotangulia nchini Spian.Hakuna kielezo rasmi kwanini Eto’o hatakuwa uwanjani jioni hii.Itakumbukwa lakini kuwa Eto’o alikataa kuteremka uwanjani dakika za mwisho alipoitwa kuichezea Barcelona katika changamoto yake na Racing Santander.

Liverpool,baada ya kutwaa ubingwa msimu uliotangulia,ina kiu tena cha kuvuka hatua ya leo na inasema haitaiachia Barcelona kuwika nyumbani.

Mpambano mwengine wa kukata na shoka jioni hii ni kati ya Chelsea-mabi ngwa wa Uingereza na mabingwa wa mwaka juzi FC Porto ya Ureno wakati Valencia ina miadi na Inter Milan ya Itali.

As Roma pia ya Itali inaikaribisha nyumbani Olympique Lyon ya Ufaransa.

Chelsea ya Uingereza ikiongozwa na kocha wake Mourinho ina miadi na FC porto ya Ureno ambayo Mourinho aliiongoza kuvaa taji la Ulaya.Leo,Mourinho anataka kuivua taji la msimu huu Porto na mapema.Miaka 2 nyuma Porto iliikomea Chelsea mabao 2:1 na mramba asali-harambi mara moja-yasema porto.

Inter Milan ya Itali imeramba ushindi mechi zake zote 16 za Serie A nyumbani nah ii ni rekodi katika ligi maarufu za dola kuu za dimba-Uingereza,Ujerumani,Spain na Itali.Hatahivyo, Inter inacheza na Valencia bila mfaransa staid Viera.Usalama kutokana na fujo la karibuni utakua mkali leo katika uwanja wa San Siro mjini Milan.

· Jana mabao 2 ya kipindi cha kwanza ya Raul Gonzalez na la tatu la Ruud van Nistelrooy,yalipiga msumari wa kwanza jana katika jeneza la mabingwa wa Ujerumani Bayern munich msimu huu wa champions League –Raul aliufumania mlango wa Munich mnamo dakika ya 10 ya mchezo na utamu ulipomkolea akarudi tena kwa bao la pili mnamo dakika ya 28 na hivyo kufanya idadi ya mabao yake katika champions league kuwa 56 -hiyo ni rekodi.

· Beki mshahara wa Munich, mbrazil Luicio akarejesha bao moja dakika 23 ya mchezo na ikionekana kana kwamba Real ingetoroka na mbaoa 3:1, mholanzi Mark van Bommel aliipatia Munich bao lake la pili lililofufua uhai wa mabingwa wa Ujerumani kubadili hatima yake duru ya pili nyumbani Allianz Arena machi 7.

· Van Bommel alibidi leo kuomba radhi kwa Real Madrid kwa utovu wa adabu aliouonesha uwanjani baada ya kuufumania mlango wa Real kwa bao la pili la B.Munich. Alisema, “ninapaswa kuwaomba radhi mashabikina sina kitu dhidi yao bali baadhi ya wachezaji wao.”

· Kocha wa Real Madrid Fabio Capello hakutangaza kujiuzulu kinyume na ilivyohanikiza kabla.

· Mchezaji wa zamani wa Taifa wa Ujerumani Bernd Schüster-kocha wa sasa wa Getafe huko Spian, amesema leo kwamba angependa kuwa kocha wa mabingwa wa Bundesliga-Bayern Munich.Alinukuliwa kusema, “Nadhani hakuna kocha atakaekataa kuwa kocha wa Bayern Munich. Mimi halkadhalika.”

Munich ilimpiga shoka kocha wake Felix Magath mwishoni mwa mwezi uliopita na kumuajiri kocha wa zamani mashuhuri Ottmar Hitzfeld hadi mwisho wa msimu huu.

· Nahodha wa zamani wa ujerumani na bingwa wa kombe la dunia Lothar Mattaeus ameonesha pia hamu ya kuwa kocha wa Bayern munich,klabu yake ya zamani.

 • Tarehe 21.02.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHca
 • Tarehe 21.02.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHca