Champions League : Schalke yachambuliwa kama karanga | Michezo | DW | 27.02.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Champions League : Schalke yachambuliwa kama karanga

Schalke 04 waliingia jana(26.02.2014) katika mpambano wa mzunguko wa kwanza katika Champions League dhidi ya Real Madrid wakiwa na matumaini makubwa ya kuipa changamoto timu hiyo kutoka Madrid.

Schalke vs. Madrid

Kevin Boatenga wa Schalke akiwa ameduwaa

Lakini kikosi hicho cha Schalke kilijikuta kimeduwaa kwa kuona kiwango tofauti cha uwezo kati yake na Real baada ya kuzabwa mabao 6-1 nyumbani.

Tofauti ya viwango

Ni kisago , na aibu kwa ligi ya Ujerumani. Udhalilishaji huo uliokuja wiki moja baada ya timu hiyo kuiadhiri Bayer Leverkusen inayoshika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ya Ujerumani Bundesliga kwa mabao 2-1 katika ligi hiyo , na pia baada ya Leverkusen kupokea kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya Paris St. Germain nyumbani , pia kimezusha maswali juu ya kiwango cha soka katika bundesliga, ambapo Bayern Munich , ikiongoza kwa points 19 , na Borussia Dortmund ziko kabisa katika kiwango tofauti kabisa dhidi ya timu nyingine.

Schalke vs. Madrid

Cristiano Ronaldo akishangiria bao

Kocha wa Schalke Jens Keller na wachezaji wake ambao hawana uzoefu wa kutosha amekiri kuwa hawakuwa na jibu kwa mashambulizi makali na ya kupangilia ya Real hasa katika wakati wa kushambulia kwa kushtukiza.

Ni vigumu kujilinda wakati huwezi kufika karibu ya mpira. Kushindwa kwa kiwango hicho kunaumiza, lakini ni tunastahili," nahodha Benedict Hoewedes amewaambia wandishi habari baada ya kuwashuhudia Karim Benzema, Cristiano Ronaldo na Gareth Bale kila mmoja akifunga mabao mawili.

"Tulianza vizuri, lakini tulifika wakati tuligundua kuwa , hali itakuwa ngumu", amesema Hoewedes.

"Ni ndoto kucheza dhidi ya Real Madrid lakini ni kidonge kichungu kunywa wakati inapofika wakati umezidiwa. Cristiano Ronaldo alikuwa kila mahali. Tuliona leo hasa ni kwanini yeye ni mchezaji bora wa dunia mwaka huu." ameongeza Hoewedes.

Schalke vs. Madrid

Karim Benzema (katikati)akifurahia bao na wenzake

Ukweli usiopingika

Kevin-Prince Boateng amesema kuwa Schalke,"ilifikia kikomo chake cha uwezo" wakati mchezaji wa kati Julian Draxler akaongeza: Tulipambana kadri tulivyoweza, lakini kila mara ilionekana kuwa tuko nyuma yadi moja ya wapinzani wetu."

Galatasaray vs. Chelsea Mourinho

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho

Pamoja na hayo , Schalke , ambayo inashikilia nafasi ya nne katika msimamo wa Bundesliga , imeshinda michezo mitano na kutoka sare miwili katika michezo yake saba ya mwisho na waliamini kabla ya mchezo na Real kuwa wangeweza kuwapa mabingwa hao mara nane wa Champions League changamoto kubwa.

Galatasaray vs. Chelsea

Mlinzi wa Galatasaray Chedju aliyeipatia timu hiyo bao la kusawazisha

Kwa upande mwingine timu za Uingereza zimeendelea kuonesha udhaifu katika michuano ya mwaka huu ya champions League. Wakati Arsenal London , Manchester City na Manchester United zote zimepokea vipigo, vya mabao 2-0 dhidi ya wapinzani wao katika awamu hii, matumaini yalikuwa yanawekwa kwa Chelsea ambayo hapo jana ilikuwa iko ugenini ikiumana na Galatasaray ya Istanbul.

Matokeo ni kwamba Chelsea ilishindwa kutamba licha ya kupata bao na mapema na kuishia sare ya bao 1-1.

Mwandishi.: Sekione Kitojo / rtre