1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bush awasili Sharm El Sheikh

16 Januari 2008

Rais George Bush wa Marekani awasli leo Misri kwa mazungumzo na rais Hosni Mubarak.

https://p.dw.com/p/CqO3
George Bush na mfalme AbdullahPicha: AP Photo

Rais George Bush wa Marekani anakamilisha ziara yake ya Mashariki ya kati nchini Misri hii leo bila l kufaulu kuungwamkono moja kwa moja na washirika wake wa kiarabu katika juhudi zake za kuleta amani Mashariki ya kati na kuitenga Iran na majirani zake wa Ghuba.

Adhuhuri hii, rais Bush anawasili Sharm el-Sheikh,katika mwambao wa bahari ya sham akitokea Saudi Arabia.

Katika ziara yake ya masaa 3 huko Sharm El Sheikh ,adhuhuri hii ,rais Bush anaanza moja kwa m oja mazungumzo na mwenyeji wake rais Hosni Mubarak wa Misri.Kinyume na nchi nyengine alizozitembelea kabla huko Mashariki ya kati, ziara ya George Bush nchini Misri yaangaliwa zaidi kuwa ni ya hershima tu kuliko kisiasa na kiuchumi.kituo hiki cha mwisho-Misri,ni mwisho wa ziara iliomuona rais Bush akipiga upatu na kuhanikiza kuzitaka nchi za kiarabu za ghuba kuungamkono juhudi zake za kufikia amani kati ya Israel na wapalestina hadi pale atakapoacha wadhifa wa urais hapo Januari,mwakani pamoja na kuitenga Iran.

Usuhuba na Misri umezorota kutokana na ila inazotoa Marekani kuwa Misri imeshindwa kuulinda barabara mpaka wake na mwambao wa Gaza ,unaotawaliwa wakati huu na Chama cha Hamas –chama kinachoangaliwa tangu na kambi ya magharibi hata na mshirika wake Israel kuwa ni cha „kigaidi“.

Waziri wa nje wa Marekani dr.C.Rice pamoja na Israel ameitaka Misri kufanya judi zaidi kuzuwia silaha kuingizwa kimagendo katika mwambao wa gaza.

Bunge la Marekani mwezi uliopita ilizuwia msaada wa dala milioni 100 hadi kwanza Dr.Rice atapoweza kulihakikishia kwamba Misri inafanya juhudi za kutosha kutia nta mpaka wake usivuje silaha zinazoingia Gaza.

Kwa upande mwengine, rais Hosni Mubarak, mwenyeji war ais Bush wakati huu huko Sharm el Shiekh kama viongozi wengine katika eneo hilo haridhiki na sera za george Bush tangu nchini Irak hata kuelekea Israel-hii ni kwa muujibu asemavyo Mustafa Kamal al-Sayyed,prof. wa fani ya siasa katika Chuo Kikuu cha Cairo.

Kwahivyo, Hosni mubarak atampokea rais Bush mikono miwili,lakini hataungamkono mawazo yake-alisema prof.Kamal kabla kuwasili Bush Sharm el Sheiklh.

Prof.Kamal alitaja kwamba, katika hotuba yake muhimu juzi jumatatu alioitoa baraarabu,rais Bush hakuiorodhesha Misri kuwa miongoni mwa dola zinazopiga hatua kuelekea demokrasia.

Baada ya chai ya asubuhi na aila ya kifalme ya Saudia asubuhi ya leo nje ya mji mkuu Riyadh,ndipo alipoondoka kuelkea Misri.

Mnamo siku 2 alizopitisha Saudia,mtoaji mkubwa kabisa wa mafuta duniani,alishinikiza Bush kuongezwa pato la mafuta ili kuteremsha bei chini ili kupunguza hofu za uchumi wa marekani kuzorota.rais Bush alitumai kuwa Umoja wa nchi zinazosafirisha mafuta ulimwenguni ambamo saudi Arabia ina sauti kubwa- utaelewa kwamba ikiwa mteja wao mkubwa wa m afuta akiathirika,basi hataweza kununua kwa wingi mafuta yao na gesi yao.

OPEC inakutana mjini Viemnna, Austria hapo Februari mosi.

Kuhusu utaratibu wa amani wa mashariki ya kati ambao Bush anajaribu sasa kuupalilia katika ziara hii inayomalizika leo,rais Bush amepata shida kuwsasadikisha wenyeji wake wa saudia kuungamkono kwa dhati siasa zake mbili-kuungamkono kwa nguvu juhudi zake za amani na kujitolea kuikabili kwa changamoto na Iran.

Waziri wa nje wa Saudi Arabia, Saud al Feisal, kuhusu Iran,alisema ,

„Iran ni nchi jirani na ni nchi muhimu katika Ghuba.Bila shaka ,hatuiangalii Iran kwa jicho baya.“

Si ajabu Bush akasikia maoni sawa na hayo huko Sharm el Sheikh,kutoka mwenyeji wake adhuhuri hii.