Ulaya kupigia kura marekebisho ya sheria za waomba hifadhi
10 Aprili 2024Matangazo
Makubaliano hayo mapya ya Uhamiaji na Ukimbizi yanajumuisha sheria 10 zilizoundwa baada ya miaka mingi ya mazungumzo ambayo yanalenga kuzifanya nchi za Ulaya, zote zikiwa na vipaumbele tofauti vya kitaifa, kuchukua hatua za pamoja katika suala la uhamiaji, kwa kutumia sheria sawa.
Ikiwa sheria hata moja itakosa kupitishwa, makubaliano hayo hayatafikiwa.
Makundi makuu ya kisiasa ya bunge hilo la Ulaya yameashiria kuunga mkono mkataba huo. Vyama vya mrengo mkali wa kulia na kushoto vinapinga baadhi ya sheria hizo.
Mashirika ya misaada na yasiyo ya kiserikali pia yamejitokeza kupinga makubaliano hayo, ambayo yanayaona kama nia ya kufanya kuwa vigumu zaidi kwa wakimbizi kutafuta hifadhi na ulinzi.