Bundesliga uwanjani | Michezo | DW | 27.10.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Bundesliga uwanjani

Baada ya ushindi mnono katikati ya wiki ,Borussia Dortmund na Schalke 04 zinarejea katika kinyang'anyiro cha nyumbani ili kuziba mwanya nyuma ya viongozi wa ligi ya Ujerumani ,Bundesliga ,Bayern Munich.

DORTMUND, GERMANY - OCTOBER 20: Ibrahim Affelay (L) of Schalke scores his team's first goal during the Bundesliga match between Borussia Dortmund and FC Schalke 04 at Signal Iduna Park on October 20, 2012 in Dortmund, Germany. (Photo by Alex Grimm/Bongarts/Getty Images)

Dortmund ilipopambana na Schalke Wiki iliyopita

Bayern Munich inashikilia uongozi kwa points tano katika Bundesliga na wanaikaribisha Bayer Leverkusen katika uwanja wa Allianz Arena kesho Jumapili, wakati Schalke 04 iko nyuma ya viongozi hao kwa points saba, na Dortmund ambayo inashikilia nafasi ya nne katika msimamo wa ligi iko points 12 nyuma ya viongozi hao.

Bayern ilipata ushindi wa bao 1-0 katika kinyang'anyiro cha Champions League dhidi ya Lille ya Ufaransa siku ya Jumanne, na kulazimisha timu tatu katika kundi la F kuwa na points sita kila mmoja , pamoja na Valencia na BATE Borisov.

Bayern Munich's Brazilian defender Dante reacts during the German first division Bundesliga football match FC Schalke 04 vs FC Bayern Munich on September 22, 2012 in Gelsenkirchen, western Germany. Bayern Munich won the match 0-2. AFP PHOTO / PATRIK STOLLARZ RESTRICTIONS / EMBARGO - DFL RULES TO LIMIT THE ONLINE USAGE DURING MATCH TIME TO 15 PICTURES PER MATCH. IMAGE SEQUENCES TO SIMULATE VIDEO IS NOT ALLOWED AT ANY TIME. FOR FURTHER QUERIES PLEASE CONTACT DFL DIRECTLY AT + 49 69 650050. (Photo credit should read PATRIK STOLLARZ/AFP/GettyImages)

Mchezaji wa Bayern Munich Dante

Lakini Bayern imeanza vizuri msimu huu wa Bundesliga na wanawania ushindi wao wa mchezo wa tisa mfululizo katika Bundesliga , baada kuvunja rekodi ya kushinda michezo saba baada ya kuiangusha Fortuna Dusselsdorf Jumamosi iliyopita.

Hamasa Dortmund

Mabingwa wa Ujerumani Borussia Dortmund wana miadi na Freiburg leo Jumamosi (27.10.2012) wakitiwa hamasa na ushindi wao mnono wa mabao 2-1 dhidi ya Real Madrid, siku ya Jumatano.

Borussia wamefuta majonzi ya kupigwa mweleka wa mabao 2-1 na watani wao wa jadi Schalke 04 mwishoni mwa juma lililopita, wakati mlinzi wa timu ya taifa ya ujerumani Marcel Schmelzer alipopachika bao la ushindi katika dakika ya 64 na kuwaondoa Rela katika uongozi wa kundi D la champions League.

Schalke 04 iko nyumbani dhidi ya Nuremberg ambayo inashikilia nafasi ya 15. Schalke inaogelea katika furaha ya ushindi mnono wa mabao 2-0 dhidi ya Arsenal London.

"Baada ya ushindi katika mchezo wa watani wa jadi wa bonde la Ruhr, ushindi dhidi ya Arsenal ulikuwa ni furaha mara mbili , na najisikia fahari kuwa katika kokosi hiki", amesema mchezaji wa kati wa Schalke na nahidha wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 21 Lewis Holtby.

Eintracht Frankfurt inayoshikilia nafasi ya pili inaendelea kuwa timu inayoshtua na kutisha msimu huu , baada ya kupata ushindi mara sita katika michezo nane iliyocheza na kesho Jumapili inawania kuendeleza ubabe wake dhidi ya Stuttgart, ambayo ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Hamburg wiki iliyopita.

Mwishoni mwa msimamo wa ligi , VFL Wolfsburg inaikaribisha Fortuna Dusseldorf leo jioni , ikiwa chini ya uongozi wa kocha mlenzi Lorenz-Guenther Koestner baada ya klabu hiyo kuvunja ndoa na kocha wa zamani Felix Magath siku ya Alhamis.

WOLFSBURG, GERMANY - APRIL 24: Felix Magath, head coach of Wolfsburg looks on during the Bundesliga match between VfL Wolfsburg and 1. FC Koeln at Volkswagen Arena on April 24, 2011 in Wolfsburg, Germany. (Photo by Stuart Franklin/Bongarts/Getty Images) *** Local Caption *** Felix Magath;

Kocha wa zamani wa Wolfsburg Felix Magath

Wolfsburg imethibitisha kuwa Magath , mwenye umri wa miaka 59, ambaye alikuwa kocha na meneja wa timu, amejiuzulu baada ya kuwapo kazini kwa siku 586, akiiongoza timu hiyo kama kocha na imepata points tano tu msimu huu na ushindi mmoja tu katika michezo minane, ikiwa ni mwanzo mbaya kabisa kuwahi kutokea katika ligi ya Ujerumani.

Na katika Premier League nchini Uingereza,

Mchezaji wa kiungo wa Manchester United Shinji Kagawa hataonekana uwanjani kwa muda wa wiki nne baada ya kupata maumivu ya goti, wakati wa mchezo wa Champions Legue dhidi ya Braga ya Ureno katikati ya wiki.

Dortmund's Shinji Kagawa of Japan, right, scores the opening goal during the German first division Bundesliga soccer match between Borussia Dortmund and Hoffenheim in Dortmund, Germany, Saturday, Jan. 28, 2012. (AP Photo/Martin Meissner) - NO MOBILE USE UNTIL 2 HOURS AFTER THE MATCH, WEBSITE USERS ARE OBLIGED TO COMPLY WITH DFL-RESTRICTIONS, SEE INSTRUCTIONS FOR DETAILS -

Shinji Kagawa wa Manchester United , wakati akiwa Dortmund

Manchester United inakwaana kesho Jumapili na Chelsea, Everton inaonyeshana kazi katika pambano la watani wa jadi na Liverpool, wakati jioni ya leo Arsenal ina miadi na Queens Park Rangers, Manchester City inakwaana na Swansea City.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre / afpe / dpae

Mhariri : Mohammed Abdul Rahman