1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Stuttgart yaifunga Augsburg na kukamata nafasi ya tatu

23 Machi 2026

Mshambuliaji wa Ujerumani Deniz Undav alifunga mabao mawili na kutengeneza jingine wakati Stuttgart waliwafunga Augsburg 5 - 2 jana na kusonga hadi nafasi ya tatu kwenye jedwali la Bundesliga.

https://p.dw.com/p/5Atdx
Mshambuliaji wa Stuttgart Denis Undav
Mshambuliaji wa Ujerumani Deniz Undav alifunga mabao mawili dhidi ya AugsburgPicha: Robin Rudel/Pressefoto Rudel/IMAGO

Mshambuliaji wa Ujerumani Deniz Undav alifunga mabao mawili na kutengeneza jingine wakati Stuttgart waliwafunga Augsburg 5 - 2 jana na kusonga hadi nafasi ya tatu kwenye jedwali la Bundesliga. Ushindi huo umewapa Stuttgartpengo la pointi tatu dhidi ya nambari nne RB Leipzig.

Katika mechi nyingine, Mainz iliendeleza safari ya kuiondoa eneo la mkia na kufika nafasi salama za katikati mwa jedwali kwa ushindi wa 2 - 1 nyumbani dhidi ya Eintracht Frankfurt. Wako nafasi ya 11 katika Bundesliga, pointi sita juu ya eneo la mechi ya mchujo ya kushushwa daraja.

Kwingineko, St Pauli walipoteza 2 - 1 nyumbani dhidi ya Freiburg na kujikuta katika hatari ya kushuka daraja. St Pauli wako katika nafasi ya mechi ya mchujo ya kushuka daraja, pointi mbili nyuma ya Cologne ambao, walimfuta kocha Lukas Kwasniok jana Jumapili. Kocha msaidizi Rene Wagner amechukua usukani kwa kipindi cha mpito.