1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRISBANE: Daktari aruhusiwa kuondoka Australia

28 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBeM

Daktari wa Kihindi aliezuiliwa Australia kuhusika na majeribo mawili ya kigaidi nchini Uingereza, anaruhusiwa kuondoka Australia.Majeribio hayo ya kigaidi yalishindwa kufanikiwa.

Waziri wa Uhamiaji wa Australia,Kevin Andrews amesema,baada ya kupata ushauri,ikiwa ni pamoja na wa Idara ya Polisi ya Australia,ametoa taarifa kuwa Dkt.Mohammed Haneef anaweza kuondoka Australia.

Dkt.Haneef alitolewa jela siku ya Ijumaa,baada ya kuondoshwa kwa mashtaka ya kuhusika na njama ya kigaidi nchini Uingereza.