1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Borussia  Dortmund yaendelea  kukaa  kileleni 

Sekione Kitojo
21 Januari 2019

Borussia  Dortmund yaendelea  kukaa  kileleni  mwa msimamo  wa Bundesliga, Bayern yaja  kwa  kasi kuisaka BVB

https://p.dw.com/p/3BukT
Fußball Bundesliga 18. Spieltag | RB Leipzig vs. Borussia Dortmund Witsel
Picha: picture-alliance/dpa/J. Woitas

 

Ligi  ya  Ujerumani  Bundesliga, Borussia  Dortmund imemaliza wiki  ya  kwanza  ya  Bundesliga  katika  mwaka  huu 2019  ikiwa  bado  imeendelea  kuweka  mwanya  wa  pointi  sita  juu ya  mabingwa  watetezi  Bayern Munich wakati  mbio  za  kufukuzia ubingwa  wa  Ujerumani  msimu  huu  ukiendelea  kuleta  msisimko mkubwa. Borussia  Dortmund  ilitoka  na  ushindi  wa  bao 1-0  dhidi ya  RB Leipzig  siku  ya  Jumamosi  kufuatia  kipigo  ilichotoa Bayern  Munich  cha  mabao 3-1  dhidi  ya  Hoffenheim siku  ya Ijumaa.

Fußball Bundesliga 18. Spieltag | RB Leipzig vs. Borussia Dortmund
Wachezaji wa Borussia Dortmund wakipambana na RB Leipzig Picha: Getty Images/Bongarts/K. Hessland

Leon Goretzka , ambaye  alipachika  mabao  mawili  katika  ushindi wa  Bayern dhidi  ya  Hoffenheim , mzaliwa  wa  mji  wa  Bochum alisema  baada  ya  mchezo  huo  kuwa  ushindi  wa  kwanza  baada ya  mapumziko  ya  majira  ya  baridi ni  muhimu, kuendelea  katika njia  sahihi. Msako  bado  unaendelea  kuisaka  Dortmund, aliongeza.

Nico Schulz , ambaye  alifunga  bao  pekee  la  Hoffenheim  katika mchezo  huo , alisema  Kingsley Coman  amemsamehe kwa kumfanyia  faulo  mbaya  kabisa  ambayo  ilimuweka  nje  ya  uwanja Mfaransa  huyo  kwa  miezi  mitatu. Kulikuwa  na hali  ya  kupendeza wakati  wachezaji  hao  wakikumbatiana  wakati wa  mapumziko  siku ya  Ijumaa  wakati Schulz  alipomkumbatia  Coman na  kuomba msamaha  kwa  rafu  ile  aliyofanya  ambayo  ilimuweka  mchezaji huyo  wa  pembeni  wa  Bayern  nje  ya uwanja  kwa  muda  mrefu.

1. Bundesliga | TSG 1899 Hoffenheim vs. FC Bayern München |
Wachezaji wa Bayern wakishangiria ushindi dhidi ya HoffenheimPicha: Reuters/R. Orlowski

Eintracht  Frankfurt  inaelekea  katika  kufuzu  kucheza  katika Champions League  msimu  ujao, na  wanaripotiwa  kuwa  na matumaini  kwamba  wanaweza  kuendelea  kuwa  na  washambuliaji wao  watatu  wanaotia  fora  katika  kupachika  mabao  kwa  timu hiyo  msimu  ujao. Mshambuliaji Luka Jovic  akiwa  ba  mabao 13, Sebastian Haller  mabao 10  na  Ante Rebic mabao 6  wanatia  fora katika  ligi  ya  Ujerumani  Bundesliga  hivi  sasa.

Jovic mwenye  umri  wa  miaka 21, ambaye  anaongoza  ufungaji katika  ligi  hadi  sasa, ana  mkataba  wa  kuazimwa  na  Frankfurt wanasema  wanataka  kulipa  euro  milioni  6 ambazo Benfica inataka  kupata  saini  ya  mchezaji  huyo  Mcroatia mwenye  umri wa  miaka  21.

Bundesliga 18. Spieltag | Eintracht Frankfurt vs. SC Freiburg
Luka Jovic wa Eintracht Frankfurt (kushoto) akipambana na Janik Haberer wa FreiburgPicha: Imago/J. Huebner

Frankfurt yachachamaa

Frankfurt  iko  katika  nafasi  ya  tano ikiwa  na  pointi 30, pointi moja  nyuma  ya  timu  iliyoko  katika  nafasi  ya  4 , RB Leipzig yenye  pointi 31. Frankfurt  iliikandika  Freiburg  kwa  mabao 3-1 siku ya  Jumamosi.

Borussia  Moenchengladbach  iliendelea  kujiimarisha  katika  nafasi ya  tatu  nyuma  ya  Bayern  Munich  kwa  kuishinda  Bayer 04 Leverkusen  kwa  bao  1-0,  wakati VFL Wolfsburg  ilishindwa kutamba mbele  ya  Schalke 04, pale  ilipozabwa  kwa  mabao 2-1 ugenini  na  kushindwa  kusogea  na  kukaribia  nafasi  ya  kucheza katika  Champions League.

Schalke  sasa  imechupa  kutoka  nafasi ya  14  na  kutua  katika  nafasi ya  12 , ikiwa  na  pointi  21. Ikumbukwe  kwamba  Schalke  bado  imo  katika  eneo  la  hatari  ya kushuka  daraja  kwani  inapishana  kwa  pointi 6 tu na  timu zilizoko katika  eneo  hilo.

Fußball Bundesliga - Bayer Leverkusen v Borussia Mönchengladbach
Kevin Volland wa Leverkusen (kushoto) na Michael Lang wa Borussia Moenchengladbach (kulia)Picha: Imago/Uwe Kraft

Wakati  huo  huo Schalke 04  imemuondoa nahodha  wake  na mlinda  mlango Ralf Fäemann kwa  ajili  ya  pambano  la  Jumapili dhidi  ya  Wolfsburg , mwezi  mmoja  kabla  ya  pambano  lake  la Champions  League  katika  awamu  ya  mtoano  wa  timu  16 dhidi ya  Manchester City.  Faemann  mwenye  umri  wa  miaka  30 , ambaye  ameitumikia  Schalke  katika  michezo 228  ya  Bundesliga na  ambaye  alianzia  kutoka  utotoni  katika  klabu  hiyo, nafasi yake  ilichukuliwa  na  mlinda  mlango  wa  timu  ya  taifa  ya Ujerumani  chini  ya  miaka  21 Alexander Nuebel katika  mchezo  wa kwanza  wa  klabu  hiyo  jana  baada  ya  mapumziko  ya  majira  ya baridi.

 

Mwandishi: Sekione  Kitojo / dpae / afpe / rtre / ape

Mhariri: Josephat Charo