Bomu laua watu Karachi | Habari za Ulimwengu | DW | 15.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Bomu laua watu Karachi

KARACHI:

Polisi nchini Pakistan inasema kuwa kwa uchache watu wanane wameuliwa na wengine 40 kujeruhiwa katika shambulio la bomu katika mji wa kusini wa bandari wa Karachi. Maafisa wanasema kuwa bomu lilikuwa limefungwa katika pikipiki na kukanusha habari za awali kuwa lilikuwa shambulio la kujitolea mhanga.Pakistan imekumbwa na ghasia tangu kuuliwa kwa kiongozi wa upinzani Benazir Bhutto wakati wa mkutano wa hadhara mwezi jana.Rais wa Pakistan Perves Musharraf amehakikisha kuwa uchaguzi mkuu utafanyika Febuari 18 licha ya kuuliwa kwa Bhutto.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com