Bolt akaribia kutimiza ndoto yake
8 Januari 2018Matangazo
Hata hivyo, bingwa huyo wa Olimpiki na dunia alikiri kuwa anapendelea kuichezea timu anayoipenda zaidi ya Manchester United.
Bolt mwenye umri wa miaka 31 ameliambia gazeti la Sunday Express kuwa atafanya majaribio mwezi Machi katika klabu ya BVB kabla ya kuamua kama ataweza kucheza kandanda. Mjamaica huyo anasema kama watasema yuko sawa, na kwamba anahitaji kufanya mazoezi, atafanya hivyo. Lakini kwa sasa ana hofu kwa sababu kandanda ni kitu tofauti na riadha na itabidi achukua muda ili kuzoea.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP/Reuters
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman