Blair ahojiwa kuhusu Iraq | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 30.01.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Blair ahojiwa kuhusu Iraq

Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair ametetea uamuzi wake wa kushiriki katika uvamizi dhidi ya Iraq ulioongozwa na Marekani katika mwaka 2003.

default

Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair ambaye alihojiwa siku ya Ijumaa kwa kuhusika kwake na uvamizi dhidi ya Iraq.

LONDON:

Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair ametetea uamuzi wake wa kushiriki katika uvamizi wa Iraq ulioongozwa na Marekani katika mwaka 2003. Akizungumza mbele ya tume inayochunguza sababu za kuingia vita vya Iraq,Blair alisema kuwa hajuti kusaidia kumuondosha madarakani kiongozi wa Iraq Saddam Hussein. Amesema kufuatia shambulio la kigaidi la Septemba 11 nchini Marekani, ilikuwa dhahiri kuwa serikali zenye silaha za maangamizi zisistahimiliwe tena. Uchunguzi unaofanywa hivi sasa unataka kujua iwapo Blair alikuza ripoti za upelelezi zilizodai kuwa Iraq ilikuwa na silaha za maangamizi na iwapo uvamizi wa Iraq umekiuka sheria ya kimataifa.

 • Tarehe 30.01.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/LnP2
 • Tarehe 30.01.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/LnP2
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com