1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benki ya BRICS inaweza kusaidia miradi ya Afrika

24 Agosti 2023

Rais wa Benki ya New Development iliyoanzishwa na mataifa wanachama wa kundi la BRICS, Dilma Rousseff, amesema benki hiyo inaweza kufadhili miradi itakayochangia katika kukabiliana na changamoto za dharura zaidi Afrika.

https://p.dw.com/p/4VXiK
Brasilien Ex-Präsident Fernando Collor de Mello
Picha: Eraldo Peres/AP Photo/picture alliance

Rais huyo wa zamani wa Brazil amesema kwenye hotuba yake kwamba mataifa ya BRICS ni washirika wazuri kwa Afrika na kuongeza kuwa benki hiyo iliyoanzishwa mwaka 2015 itafadhili miradi ya miundombinu ya kawaida na ya kidijitali pamoja na ile ya elimu.

Rousseff ni miongoni mwa wanaohudhuria mkutano wa kilele wa BRICS unaomalizika leo mjini Johannesburg nchini Afrika Kusini.