1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beni yatangaza visa vitatu vya Ebola

Lilian Mtono
14 Aprili 2020

Wakati wakaazi wa Beni walikuwa wanatarajia kutangaza kutokomezwa kwa homa ya ebola katika mji wao, ndoto hiyo imepotea baada ya kutangazwa kwa visa vipya vitatu vya maambukizi ya ugonjwa huo.

https://p.dw.com/p/3arns
Symbolbild Masernkrise
Picha: picture-alliance/AP Photo/J. Delay

Katika juhudi za kuepusha maambukizi zaidi baraza la usalama la mji wa Beni limeamua kuwaweka karantini madaktari wa hospitali alikopatiwa matibabu mgonjwa aliefariki kwa ebola wiki iliyopita.

Maambukizi hayo yamewakatisha tamaa wakaazi wa eneo hili, waliokuwa wanategemea kutokomezwa kwa homa ya Ebola katika eneo lao, wakati ambapo wanakabiliana pia na virusi vya corona, ambapo mapaka sasa mji wa Beni umerikodi visa viwili vya kirusi hicho.

Akizungumza na wanahabari kwenyi ofisi yake, Meya wa Beni Bwanakawa Masumbuko Nyonyi akiwa mwenyi huzuni kuhusu visa vipya vya Ebola alisema, ili kuepuka maambukizi zaidi, watabibu kwenye hospitali ya Nyankunde pamoja na zahanati ya Horizon Beni, wamewekwa karantini kwa kipindi cha siku ishitini na moja mfululizo.

Symbolbild Masernkrise
Hii ni picha ya mwaka 2019 ya mwathirika wa virusi vya Ebola, akizikwa na watumishi wa afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya CongoPicha: picture-alliance/AP Photo/J. Delay

Meya Bwanakawa Nyonyi alisema"Hesabu ya siku hizo ishirini na moja inaanza leo na tunayo matumaini kuhusu hospitali ya Nyankunde kwani watabibu kadhaa au tuseme wote wa hospitali hiyo walipatiwa mapema chanjo dhidi ya Ebola na kwa hiyo matatizo ni machache kabisa. Na kituo cha pili alikopatiwa matibabu marehemu, kituo cha Afya Horizon Beni, nacho kinafungwa kwa kipindi cha siku ishirini na moja."

Aidha Meya huyo wa Beni aliwahamasisha wakaazi wa mji wake, kuheshimu kanuni za kujikinga dhidi ya ebola, akiwakumbusha wakaazi wake, kwamba virusi vya ebola vinabaki katika mwili ya mtu aliepona, kwa kipindi cha siku mia tano, na virusi hivyo hua vinaambukizwa wakati wa tendo la ndoa. Huyu tena Meya wa Beni.

Soma Zaidi:DRC yatarajia kutangaza mwisho wa Ebola mwezi April

Ifahamike kuwa, wakaazi wa Beni wanakabiliana upya na homa ya ebola, huki kukiwa pia na mripuko wa virusi vya corona, mji wa Beni ukiwa na wagonjwa wawili wa ugonjwa huo, wanaopatiwa matibabu, katika vituo walimokuwa wanatibiwa wagonjwa wa ebola.

Kwa kipindi cha siku sita sasa, mkoa wa Kivu ya Kaskazini,haujashuhudia maambukizi mapya, na habari njema ni kwamba, mgonjwa mmoja kati ya wagonjwa watano walioambukizwa virusi vya corona, amepona tayari, wakati hali ya afya ya wengine wanne, inaendelea vizuri.

Kupigwa marufuku kwa safari za abiria kati ya miji ya Beni, Butembo na Goma katika mkoa huu wa Kivu ya Kaskazini, kunadhaniwa na wengi,kuwa kumesaidia pakubwa, kuzuia mqambukizi zaidi.

John Kanyunyu. Beni