1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beki wa kati wa Barcelona Umtiti ajeruhiwa

Josephat Charo
9 Mei 2020

Beki wa kati wa klabu ya La Liga, Barcelona, Samuel Umtiti amepata jeraha siku moja tu baada ya timu kurejea katika mazoezi.

https://p.dw.com/p/3byb5
Championsleague FC Barcelona vs AS Roma
Picha: Reuters/J. Medina

Klabu hiyo imetoa taarifa fupi Jumamosi (09.05.2020) kuthibitisa jeraha la Umtiti kwenye msuli wa mguu wake wa kulia.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 amekumbwa na majeraha tangu aliposaini mkataba na Barcelona akitokea Lyon mwaka 2016, akianza mechi tisa tu msimu huu.

Ligi kuu ya Uhispania La Liga inatumai kuanza tena Juni 13 baada ya kusitishwa kutokana na janga la virusi vya corona.

Barcelona hawajatangaza tarehe ya uwezekano wa Umtiti kurejea.

Huku Jean-Clair Todibo akiwa katika klabu ya Schalke kwa mkopo, kukosekana kwa Umtiti kutawaacha vinara wa La Liga, Barcelona, na mabeki watatu wa kati: Gerald Pique, Clement Lenget, na chipuikizi kutoka timu ya vijana, Ronald Araujo.

(dpa)