BEIRUT : Raia sita Walebanon wafunguliwa mashtaka | Habari za Ulimwengu | DW | 12.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIRUT : Raia sita Walebanon wafunguliwa mashtaka

Hakimu mjini Beirut amefunguwa mashtaka dhidi ya wananchi sita wa Lebanon kuhusiana na njama za kuripuwa treni mbili za Ujerumani katika kipindi cha majira ya kiangazi mwaka jana.

Hakimu huyo amependekeza adhabu ya vifungo vya maisha na kazi ngumu kwa watuhumiwa wote sita watano kati yao wakiwa wanashikiliwa nchini Lebanon.Mtuhumiwa mwengine wa sita ambaye anashikiliwa nchini Ujerumani atashtakiwa mwenyewe akiwa hayupo.

Kwa mujibu wa sheria ya Lebanon watuhumiwa hao hawawezi kupelekwa Ujerumani kwa ajili ya kushtakiwa.Watuhumiwa hao wanashtakiwa kutokana na kugundulika kwa mabomu yaliotengenezwa kienyeji na kuwekwa kwenye treni mbili katika jimbo la Ujerumani magharibi la North-Rhine Westfalia mwezi wa Julai mwaka jana.

Mabomu hayo yalikuwa na hitilafu na yalishindwa kuripuka.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com