1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut. Mapigano yazuka tena.

28 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBxR

Juhudi nyingine za usitishaji wa mapigano zimevunjika kaskazini ya Lebanon wakati mapigano mapya yalipozuka kati ya jeshi la Lebanon na wapiganaji katika kambi ya wakimbizi ya Wapalestina.

Milio ya bunduki ilisikika kuzunguka kambi ya wakimbizi ya Nahr al-Bared wakati makundi ya Kipalestina ikiwa ni pamoja na Fatah na Hamas yakijaribu kufikia suluhisho la kisiasa ili kumaliza mapigano hayo.

Majeshi ya Lebanon yameizunguka kambi hiyo na yanasemekana kuwa yanajitayarisha kulizingira eneo hilo kwa muda mrefu.

Maafisa wa umoja wa mataifa wamesema kuwa zaidi ya wakimbizi 20,000 wamekimbia kambi hiyo tangu mapigano hayo yazuke wiki moja iliyopita, lakini maelfu kadha wamebaki ndani ya kambi hiyo.

Maafisa wa Lebanon wanadai kuwa wapiganaji wajisalimishe.