Bei ya mafuta nchini Zimbabwe yapanda mara mbili | Matukio ya Afrika | DW | 24.06.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Bei ya mafuta nchini Zimbabwe yapanda mara mbili

Bei ya mafuta  nchini Zimbabwe  zitapanda  kwa  hadi asilimia 152, idara ya udhibiti wa  bei  za  nishati imesema, baada  ya  serikali  kuondoa kiwango  maalum kilichowekwa tangu mwezi Machi.

Bei ya mafuta  nchini Zimbabwe  zitapanda  kwa  hadi asilimia 152 leo, idara ya udhibiti wa  bei  za  nishati imesema, baada  ya  serikali  kuondoa kiwango  maalum kilichowekwa tangu mwezi Machi.

Mara  ya  mwisho  nchi  hiyo ya  kusini  mwa  Afrika iliposhuhudia ongezeko  la  juu  la  bei  la  mafuta, Januari mwaka  2019, kulizuka  maandamano yaliyokuwa  na ghasia, na  kusababisha  zaidi  ya  watu 17  kuuwawa baada  ya  ukandamizaji uliofanywa  na  majeshi  ya usalama. 

Zimbabwe  tayari  inapitia  mzozo  mbaya  kabisa  wa kiuchumi  katika  muongo  mmoja , kukiwa  na  ughali  wa maisha  wa  kiwango  cha juu, na ukosefu wa  dawa  na chakula. Bei ya mafuta  itapanda kwa  dola  za Zimbabwe 71.62 sawa  na  dola  za  Marekani 1.25 kwa  lita, kutoka dola  ya  Zimbabwe  28.96.