1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern yarejea kileleni

Bruce Amani
12 Desemba 2016

Imekuwa wikendi nzuri kwa Borussia Moenchengladbach ambao walipata ushindi wao wa kwanza katika wiki 11 na kumwondolea shinikizo kocha Andre Schubert

https://p.dw.com/p/2U98j
Deutschland Fußball Bundesliga Bayern München vs. VfL Wolfsburg
Picha: picture-alliane/AP Photo/M. Schrader

Gladbach waliwafunga Mainz bao moja kwa sifuri. Matokeo hayo yamewasogeza Gladbach katika nafasi ya 12, pointi moja nyuma ya Mainz. Bayer Leverkusen ilipata ushindi wa moja bila dhidi ya Schalke kupitia bao la kichwa la Stefan Kiessling. Matokeo hayo yamewaweka timu hiyo katika nafasi ya nane

Siku ya Jumamosi, Bayern Munich ilirejea kileleni mwa ligi baada ya kuicharaza Wolfsburg mabao matano kwa bila. Leipzig na Bayern sasa zina pointi 33 kila mmoja lakini vijana wa Carlo Ancelotti wana faida ya mabao. Timu hizo zitakutana Desemba 21.

Rekodi ya RB Leipzig ya kutoshindwa katika mechi 13 mfululizo hatimaye ilifikia kikomo baada ya kufungwa bao moja kwa bila na Ingolstadt. Leipzig na Bayern sasa zina pointi 33 kila mmoja lakini vijana wa Carlo Ancelotti wana faida ya mabao. Timu hizo zitakutana Desemba 21.

Deutschland  FC Ingolstadt - RB Leipzig  Enttäuschung
Leipzig walipoteza mechi kwa mara ya kwanza msimu huuPicha: picture alliance/SvenSimon/O. Haist

Borussia Dortmund ilikuwa inachungulia kichapo cha nne msimu huu hadi pale Marco Reus alifunga bao katika dakika ya mwisho, bao lake la kwanza katika ligi tangu aliporejea kikosini. Cologne ilikuwa imejiweka kifua mbele lakini mwishowe ikatoka sare ya moja kwa moja. BVB sasa iko katika nafasi ya sita nyuma ya vinara Bayern na Leipzig na pengo la point inane wakati Cologne ilisalia katika nafasi ya saba. Katika matokeo mengine, nambari tatu Hertha Berlin ilifungwa moja bila na Werder Bremen. Hamburg ililazwa moja bila na Augsburg wakati Darmstadt ikifungwa moja bila na Freiburg.

Refarii wa video katika Bundesliga

Na tukibakia na kandanda la hapa Ujerumani ni kuwa ligi kuu ya kandanda ya Ujerumani – Bundesliga itazindua mfumo wa marefarii wasaidizi wataokutumia video kuanzia msimu wa 2017/18. Hayo ni kwa mujibu wa meneja wa chama cha marefarii wa Ligi ya Kandanda la Ujerumani

Kutakuwa na mawasiliano kati ya refarii na msaidizi wa refarii anayetumia video. Refarii anayetumia video atakuwa na uwezo wa kushawishi maamuzi ya refarii. Mfumo huu wa video utawasaidia maafisa wakati wa kufanya maamuzi magumu kama vile penalty, mikwaju ya adhabu na maamuzi ya wachezaji kuotea.

Mwisho wa michezo kwa sasa, kwa mengi zaidi kuhusu droo ya michuano ya hatua ya 16 za mwisho ya Champions League, tembelea ukursa wetu wa  michezo, fungua dw.com/Kiswahili. Mimi ni Bruce Amani kutoka Bonn. Kwaheri kwa sasa

Mwandishi: Bruce Amani/DPA/AFP
Mhariri: Yusuf Saumu