Bayern yaonywa kujipiga kifua, msimu bado mbichi | Michezo | DW | 28.09.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Bayern yaonywa kujipiga kifua, msimu bado mbichi

Afisa Mkuu Mtendaji wa klabu ya Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenige, ameonya kuwa mwanzo mzuri wa klabu hiyo haufai kuviingia vichwani au wakumbwe na kitisho cha kurudia masihara ya msimu uliopita.

Fußball Bundesliga 5. Spieltag: FC Bayern München - VfL Wolfsburg am 25.09.2012 in der Allianz Arena in München (Oberbayern). Torschütze Mario Mandzukic (l-r), Xherdan Shaqiri und Franck Ribery von München freuen sich über das 2:0. Foto: Andreas Gebert/dpa (Achtung: Hinweis zur Bildnutzung! Die DFL erlaubt die Weiterverwertung von maximal 15 Fotos (keine Sequenzbilder und keine videoähnlichen Fotostrecken) während des Spiels (einschließlich Halbzeit) aus dem Stadion und/oder vom Spiel im Internet und in Online-Medien. Uneingeschränkt gestattet ist die Weiterleitung digitalisierter Aufnahmen bereits während des Spiels ausschließlich zur internen redaktionellen Bearbeitung (z.B. via Bilddatenbanken).)

5. Spieltag FC Bayern München - VFL Wolfsburg

Bayern wameshinda mechi zao zote tano za mwanzo msimu huu katika ligi ya bundesliga na wana tofauti ya pointi nane mbele ya mahasimu wao ambao ni mabingwa watetezi Borussia Dortmund. Rummenige amesema ataukanyaga mguu chini na hataanza kujivunia.

Karl-Heinz Rummenigge anasema lengo lao msimu huu ni kutwaa taji la nyumbani - Bundesliga

Karl-Heinz Rummenigge anasema lengo lao msimu huu ni kutwaa taji la nyumbani - Bundesliga

Hali ilikuwa kama hiyo msimu uliopita baada ya mechi sita, tofauti baina ya timu hizo mbili ilikuwa point inane kabla ya Dortmund kurejea kwa kishindo na kutetea taji lake. Rummenige anasema lengo lao kuu ni kutwaa taji la BUNDESLIGA.

Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Löw, ameelezea furaha yake kufuatua kurejea katika hali nzuri na kupona jeraha kiungo Bastian Schwiensteiger kabla ya ratiba ya mwezi ujao ya mechi za kufuzu katika dimba la dunia.

Ujerumani itasafiri hadi Dublin kupambana na Jamhuri ya Ireland mnamo Oktoba 12 na kisha kuwaalika Sweden siku nne baadaye mjini Berlin katika mchuano wa kundi C kwa mechi za kufuzu kwa kombe la dunia 2014 nchini Brazil. Kiungo huyo wa Bayern Munich Schweinsteiger, mwenye umri wa mika 28, hajaichezea nchi yake tangu mchuano wa nusu fainali wa dimba la UEFA EURO 2012 ambapo walishindwa na Itali mjini Warsaw mwezi Juni.

Joachim Loew ameangazia macho yake katika fainali za kombe la dunia mwaka wa 2014

Joachim Loew ameangazia macho yake katika fainali za kombe la dunia mwaka wa 2014

Kisha akakosa mechi ya kirafiki waliyoshindwa magoli matatu kwa moja na Argentina nyumbani na mechi za mwanzo za kufuzu kwa kombe la dunia ambazo walishinda zote dhidi ya Visiwa vya Faroe na Austria.

Lakini, hata hivyo, amekuwa na mwanzo mzuri na Bayern msimu huu, ikiwa ni pamoja na kufunga magoli mattau na moja katika ushindi wao wa mbili wka moja dhidi ya Valencia katika mchuano wa kombe la Ligi ya Mabingwa.

Löw ambaye pia amemsifu Lucas Podolski kwa mwanzo wake mzuri wa maisha yake mapya katika klabu ya Arsenal na akamuunga mkono beki anayekabiliwa na shinikizo wa Borussia Dortmund Marcel Schmelzer, atakitaja kikosi chake mnamo Oktoba tano.

Tennis

Serena Williams na dadake Venus Williams ni moto wa kuotewa mbali

Serena Williams na dadake Venus Williams ni moto wa kuotewa mbali

Bingwa wa sasa wa mataji ya Wembledon na US Open, Serena Williams, amejiondoa kutoka mashindano ya China Open kwa sababu ya homa, huku dakake Venus pia akijiondoa akitaja sababu ya jeraha la mgongo.

Serena ambaye alidhihirisha umahiri wake katika mchezo wa Tennis mwaka huu kwa kupandisha idadi ya mataji yake makuu ya Grand Slam kufika 15 na kushinda dhahabu katika michezo ya Olimpiki, alijiondoa katika kinyang'anyiro hicho siku mbili kabla ya kuanza kwa duru ya kwanza.

Hilo ni pigo kubwa kwa waandalizi wa dimba hilo la Beijing kwa sababu mwana Tennis huyo anayeorodheshwa nambari nne ulimwenguni, na ambaye tayari amefuzu kwa vinyang'anyiro vya kumalizia msimu vya Ubingwa wa WTA mjini Istanbul, Uturuki mwezi ujao, ni mmoja wa wachezaji bora zaidi wa dimba hilo.

Mwandishi: Bruce Amani/DPA/AFP/Reuters
Mhariri: Miraji Othman