Bayern yaichapa Chelsea magoli 3-0 katika Champions League | Michezo | DW | 26.02.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Bayern yaichapa Chelsea magoli 3-0 katika Champions League

Klabu ya Bayern Munich imeitandika klabu ya Chelsea ya England mabao 3-0 katika mechi ya 16 bora ya kuwania ubingwa wa vilabu barani Ulaya huku Gnabry akitupia mabao mawili.

Katika michuano ya vigogo 16 wa soka wanaowania ubingwa wa ulaya, Bayern Munich imeifunga Chelsea magoli 3-0. Magoli hayo yalipishana kwa dakika kadhaa na yalitiwa na Serge Gnabry na Robert Lewandowski. Mabingwa hao wa Ujerumani, walionyesha udhibiti mkali wa asilimia 63 dhidi ya wenyeji wao katika uwanja wa Stamford Bridge. Kocha wa Bayern Hansi Flick amesema yalikuwa ni matokeo mazuri kwa upande wao. Timu yake ilicheza mchezo mzuri kwa umakini kama walivyojipanga. Kwa matokeo hayo, Bayern wanakaribia kuongeza mkataba wa Flick. Mwenyekiti wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge alimpatia kocha huyo zawadi ya siku yake ya kuzaliwa jijini London na kuashiria kumwongezea wino.