1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern wamsajili Coutinho

19 Agosti 2019

Bayern Munich Jumatatu wamekamilisha usajili wa Mbrazili Philippe Coutinho kutoka Barcelona kwa mkopo wa msimu mzima. Klabu hiyo ya Ujerumani imesema Coutinho alikamilisha vipimo vya kiafya Jumapili.

https://p.dw.com/p/3O8Tw
Fußball Spieler Philippe Coutinho bei Bayern München
Picha: AFP/C. Stache

Baada ya vipimo hivyo Coutinho alitia saini mkataba utakaomuweka hapo Allianz Arena hadi mwezi Juni mwaka 2020 ambapo watakuwa na fursa pia ya kumsajili kwa mkataba wa kudumu iwapo watakuwa wameridhishwa naye.

Barcelona wamesema mabingwa hao wa Ujerumani watawalipa yuro milioni 8.5 kama ada na pia wataulipa mshahara wa mchezaji huyo. Coutinho atavaa fulana nambari 10.

Coutinho ni mchezaji wa kimataifa

Mashabiki wa klabu hiyo wanahisi huenda akawa chachu ya mafanikio msimu huu.

Fußball Vertragsunterzeichnung Philippe Coutinho
Coutinho amejiunga kwa mkopo kutoka BarcelonaPicha: picture-alliance/SvenSimon

"Ninafurahi sana kwa kuwa sasa tumekiongezea nguvu kikosi chetu. Nilishangaa sana baada ya wachezaji wachache sana kusajiliwa lakini sasa baada ya mchezaji huyu nyota kusajili nina matumaini tutayafikia malengo tuliyoweka. Nasikitika hakuwepo Ijumaa lakini nafikiri ameiongezea nguvu Bayern," alisema Stefan Obermeier.

Shabiki mwengine anasema Coutinho ni mchezaji wa kimataifa.

"Ni wazi kwamba huyu ni mchezaji wa kiwango cha kimataifa, yani ni kile tulichokikosa tu kwenye mechi ya Ijumaa tulipotoka sare. Iwapo kuna mshambuliaji mwengine wa haiba ya juu tutakayempata basi kikosi kitakuwa kimekamilika na tutakuwa na matumaini kwa msimu huu," alisema Jannik Schutzmeister.

Mbrazili huyo lakini hakuyafikia matarajio ya wengi baada ya kujiunga na Barcelona kutoka Liverpool mwaka jana.