1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Schweinsteiger ajiunga na Manchester United

12 Julai 2015

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30 alikuwa ameieleza klabu yake kuwa hakutaka kuurefusha mkataba wake baada ya ulioko sasa kukamilika mwisho wa mwaka ujao.

https://p.dw.com/p/1FxS9
Fußball Bundesliga 34. Spieltag Bayern München vs. FSV Mainz 05
Picha: picture-alliance/dpa/M. Müller

Hata hivyo mkurugenzi mkuu mtendaji wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amekiri kuwa tayari Manchester United wamewasiliana nao. Schweinsteiger amecheza mechi 536 tangu ajiunge na klabu hiyo ya Bayern mwaka wa 2002.

Rummenigge amesema inahuzunisha sana kwani Bastian alikuwa ni kigogo wa timu ya Bayern na wangemtaka sana aendelee kuwachezea mabingwa hao.

Schweinsteiger amekuwa Bayern Munich kwa miaka 17. "ametufanyia mambo mengi mazuri tu kwa hivyo alipoomba ruhusa ya kuondoka hatukuwa na budi'' Alisema Rummenige

''Kwetu ni heshima kwani ametuhudumia kwa miaka 17 kwa hivyo tukamuacha aendee akastaafie Uingereza'' alisema Rummenigge

Kocha wa Man Utd Louis van Gaal amekuwa shabiki wa Schweinsteiger tangu mwaka wa 2009 – 2011 wakati alipoingoza klabu hiyo katika fainali ya Champions League ya mwaka wa 2010.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Mohamed Dahman