1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern, Chelsea na kibarua cha barani Ulaya

9 Machi 2015

Bayern Munich na Chelsea zitataraji kumalizia vibarua walivyo navyo ili kufuzu katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, baada ya timu zote kutoka sare katika mechi zao za ugenini za mkondo wa kwanza

https://p.dw.com/p/1EniD
UEFA Champions League Arjen Robben David Alaba Schachtar Donezk FC Bayern München Ukraine
Picha: picture-alliance/dpa/Andreas Gebert

Chelsea, iliyoshinda Kombe la 2012, ilipata goli la ugenini katika sare ya 1-1 na Paris St Germain wakati mabinhwa wa 2013 Bayern Munich wakitoka sare ya bila na Shakhtar Donetsk mjini Lviv.

Kesho Jumanne, Porto itakutana na Basel baada ya sare ya 1-1 nchini Uswisi wakati Real Madrid wakitaraji kuwa faida yao ya mabao mawili kwa sifuri itatosha kuwapa tikiti ya robo fainali nyumbani kwa Schalke.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/reuters
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman