Bayern bado yashikilia usukani | Michezo | DW | 23.11.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Bayern bado yashikilia usukani

Bayern Munich, ilipata ushindi mara 12 na sare moja katika michezo 13 ya Bundesliga msimu huu, imesogea pointi nane mbele ya timu inayoifuatia Borussia Dortmund

Bayern ilishinda mabao 3-1 dhidi ya Schalke 04 siku ya Jumamosi, wakati Borussioa Dortmund iliangukia pua pale ilipokandikwa mabao 3-1 na SV Hamburg.

VFL Wolfsburg inayofuatia ikiwa katika nafasi ya tatu , ponti tano nyuma ya Dortmund , iliisambaratisha Werder Bremen kwa mabao 6-0. Hertha BSC Berlin ikaishinda Hoffenheim kwa bao 1-0 jana Jumapili na kujiweka katika nafasi nzuri ya kujisalimisha kushuka daraja. Mchezaji wa Hertha Sebastian Langkamp anathibitisha hilo.

"Nafikiri , kwamba hivi sasa tuko katika hali nzuri, kwasababu tumeweza kunyakua pointi 23, na kwamba tuko katika hali tulivu tukielekea Munich wiki ijayo, na kwamba tuko katika maeneo salama katika msimamo wa ligi, na tunajisikia vizuri. Kikosi chetu kinajiamini na nadhani , kwamba tunaweza kuendelea na hali hii, lakini ni lazima tuchukue juhudi za ziada."

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre/dpae/ afpe
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com