1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuijadili Sudan

Sudi Mnette
26 Oktoba 2021

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litafanya mkutano wa faragha Jumanne wa kuyajadili mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea nchini Sudan.

https://p.dw.com/p/42BMM
UN-Sicherheitsrat New York 2016 | Waffenembargo Libyen
Picha: Imago Images/Xinhua

Wanadiplomasia wanasema suala hilo limetokana na ombi la mataifa ya Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ireland, Norway na Estonia.

Wajumbe wa Baraza hilo ambao wanahitimisha ziara yao nchini Mali na Niger watarejea mjini  New York mchana wa leo, kwa hivyo mkutano huo umepangwa kufanyika alasiri.

Jeshi la Sudan lilijinyakulia madaraka jana Jumatatu, likamkamata waziri mkuu na maafisa wengine wa serikali ya mpito, jambo ambalo limezusha maandamano katika maeneo tofauti ya taifa hilo kwa wakati huu, yenye kushinikiza kurejeshwa kwa utawala wa kiraia.

Mapinduzi hayo ya kijeshi yanatishia kuhujumu kwa hatua zilizopigwa na taifa hilo kuelekea demokrasia.