BAGHDAD:Saddam Hussein Kuzikwa Ramadi | Habari za Ulimwengu | DW | 31.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:Saddam Hussein Kuzikwa Ramadi

Kiongozi wa zamani wa Iraq Saddam Hussein atazikwa katika mji wa Ramadi unaokaliwa na idadi kubwa ya waasi wa Kisunni magharibi mwa Baghadad na wala sio katika kijiji alikozaliwa cha Awja huko Tikrit hayo ni kwamujibu wa Familia yake.

Saddam Hussein alinyongwa hapo jana baada ya kuhukumiwa kifo kutokana na kuhusika kwake katika uhalifu dhidi ya binadamu kwenye kijiji cha Dujail alipokuwa kiongozi wa Iraq.

Vyombo vya habari vya kimataifa vilionyesha picha ya Saddam akitiwa kitanzi huku akionekana asietetereka wala kushtuka.

Baada ya Kunyongwa Maiti ya Saddam ilionekana ikiwa imewekwa ndani ya mfuko uliokuwa wazi.

Marhum Saddam Hussein aliyekuwa na umri wa miaka 69 alihukumiwa kunyongwa mwezi uliopita baada ya kukutikana na hatia ya kuhusika katika mauji ya washia kiasi 150 mwaka 1982.

Wakati huo huo nchini humo mashambulio kadhaa ya mabomu yamefanyika ambapo watu zaidi ya 60 waliuwawa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa hapo jana.Kufuatia hofu kwamba huenda wafuasi wa Saddam wakaanzisha mashambulio wanajeshi wa Marekani na Iraq wamekwekwa tayari kukabiliana na hali hiyo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com