BAGHDAD: Waumini 11 wameuawa nchini Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 07.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Waumini 11 wameuawa nchini Irak

Si chini ya waumini 115 wa madhehebu ya Kishia wameuawa katika shambulio la kujitolea muhanga nchini Irak.Vile vile zaidi ya 150 wengine wamejeruhiwa katika shambulio hilo.Wanamgambo wawili waliojitolea muhanga walijipenyeza miongoni mwa waumini waliokuwa wakipumzika ndani ya hema,kando ya barabara karibu na mji wa Hilla ulio kusini mwa mji mkuu Baghdad.Hivi sasa nchini Irak waumini wengi wapo njiani kuelekea mji takatifu wa Kerbala.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com