BAGHDAD: Watu zaidi wauawa nchini Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 28.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Watu zaidi wauawa nchini Iraq

Watu waliokuwa na bunduki wamelivizia gari la mkurugenzi mkuu wa wizara ya biashara, mjini Baghdad, nchini Iraq wakamuua pamoja na binti yake na watu wengine wawili.

Polisi wamesema watu hao walililenga kwa risasi gari la Adil Abdul-Mehsun al-Lami katika eneo la Yarmouk alipokuwa akielekea kazini.

Msemaji wa wizara hiyo amesema binti yake Adil Abdul-Mehsun alikuwa mhandisi kwenye wizara hiyo.

Watu wengine wawili waliouawa ni dereva wa gari hilo na mfanyikazi mwengine wa wizara hiyo ambayo hakutambuliwa.

Wanamgambo wanaopambana na serikali ya Iraq inayoungwa mkono na Marekani na ambayo wakuu wake wengi ni washia, wamekuwa mara kwa mara wakiwashambulia au kuwateka nyara watumishi wa serikali.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com