BAGHDAD : Watu 29 wauwawa | Habari za Ulimwengu | DW | 11.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD : Watu 29 wauwawa

Watu 29 wameuwawa leo hii katika miripuko ya mabomu nchini Iraq.

Katika shambulio moja la kujitolea muhanga maisha mripuaji kwa kutumia gari ameliripuwa lori lenye mahujaji wa Kishia waliokuwa wakirejea katika maadhimisho makuu ya kidini kutoka mji mtakatifu wa Karbala kusini mwa Baghdad na kuuwa watu 19 pamoja na kujeruhi wengine 25.

Mripuaji mwengine wa kujitolea muhanga maisha amejiripuwa katika basi dogo na kuuwa watu 10 na kujeruhi 8 wakati basi hilo lilipokuwa likipita katika Chuo Kikuu cha Mustansiriya mahala ambapo pamekuwa shabaha ya mashambulizi ya Wasunni wa itikadi kali kaskazini mashariki mwa Baghdad karibu na Mji wa Sadr ambayo ni ngome kuu ya wanamgambo wa Kishia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com