1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Wanajeshi watano wauwawa.

26 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC6p

Nchini Iraq wanajeshi watano wa nchi hiyo wameuwawa na wengine 15 wamejeruhiwa katika shambulio la bomu la kujitoa muhanga kaskazini ya mji wa Baghdad. Shambulio hilo lilitokea katika kituo cha pamoja na upekuzi kati ya majeshi ya ulinzi na polisi katika mji wa Khalis katika jimbo la Diyala.

Wakati huo huo , mwanajeshi mmoja wa Marekani na kamanda wa zamani wa kituo cha jela ya kijeshi ya Marekani mjini Baghdad wameshtakiwa kwa madai ya kuwasaidia maadui.

Jeshi la Marekani limesema luteni kanali William Steele anashutumiwa kwa makosa tisa, ikiwa ni pamoja na kutoa simu za mkononi kwa wafungwa na kuwa na taarifa za siri ambazo hazikuidhinishwa.

Jeshi limesema kuwa Steele anashikiliwa nchini Kuwait, akingojea kusikilizwa kwa kesi yake ambapo ushahidi utawasilishwa kutambua iwapo suala hilo lipelekwe katika mahakama ya kijeshi.