1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Waingereza 5 wametekwa nyara Iraq

29 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBwq

Wizara ya mambo ya nje ya Uingereza imethibitisha kuwa Waingereza 5 wametekwa nyara nchini Irak. Inasemekana watu hao walikamatwa nje ya Wizara ya Fedha ya Irak.Hapo awali maafisa wa usalama wa Iraq walisema,Wajerumani 3 pia walitekwa nyara. Lakini hadi hivi sasa,ripoti hiyo haijathibitishwa na serikali ya Ujerumani.