BAGHDAD : Saddam asema kunyogwa kwake ni muhanga | Habari za Ulimwengu | DW | 28.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD : Saddam asema kunyogwa kwake ni muhanga

Rais Ahmadinejad wa Iran

Rais Ahmadinejad wa Iran

Rais wa zamani wa Iraq Saddam Hussein amesema kunyongwa kwake kunapaswa kuonekane kama ni kujitolea muhanga na amewataka wananchi wa Iraq waungane kupambana na vikosi vya Marekani nchini humo.

Ametamka hayo kwenye baruwa ya kuaga alioiandika wakati akiwa gerezani.Katika baruwa yake hiyo ambayo pia imewekwa kwenye tovuti ya mtandao Saddam pia amesema Wairaq hawapaswi kuwalaamu wananchi wa Marekani na nchi washirika wake. Timu ya mawakili wanaomtetea Saddam imesema ameagiza kundikwa baruwa hiyo muda mfupi baada ya hukumumiwa adhabu ya kifo hapo mwezi wa Novemba kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinaadamu.

Mahkama ya Rufaa imethibitisha adhabu hiyo ya kifo hapo Jumanne na kusema kwamba Saddam anapaswa kunyongwa katika kipindi kisichozidi siku 30.

Wakati huo huo habari kutoka Amman nchini Jordan zinasema kwamba naibu waziri mkuu wa zamani wa Iraq Tariq Aziz anataka kutowa ushahidi wa dharura juu ya kesi ya Saddam Hussein ya mauaji ya kimbari ya Anfal kabla ya kunyongwa kwa dikteta huyo.

Kwa mujibu wa wakili wake Aziz amemwambia kuwa ana habari muhimu anazotaka kuielezea dunia.

Mauaji ya Anfal yaliamuriwa na utawala wa Iraq dhidi ya Wakurdi mwishoni mwa miaka ya 1980.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com