BAGHDAD: Rumsfeld ametembelea vikosi nchini Irak
11 Desemba 2006Matangazo
Donald Rumsfeld anaeondoka madarakani tarehe 18 Desemba kama waziri wa ulinzi wa Marekani,alifanya ziara ya ghafla nchini Irak.Rumsfeld aliwatembelea wanajeshi wa Kimarekani katika wilaya ya machafuko ya Anbar na akawashukuru wanajeshi hao na akawaambia wakamilishe ujumbe wao nchini Irak.Robert Gates,ambae hapo zamani alikuwa kiongozi wa shirika la upelelezi la Marekani CIA,atachukua nafasi ya Rumsfeld.