BAGHDAD: Mashambulio yaendelea kuua raia nchini Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 31.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Mashambulio yaendelea kuua raia nchini Irak

Hadi watu 10 wameuawa na wengi wengine wamejeruhiwa katika mashambulio matatu ya bomu yaliolenga raia wa madhehebu ya Kishia nchini Irak.Asubuhi ya leo,mripuko uliotokea nje ya hospitali katika mtaa wa Sadr City mjini Baghdad, umeua watu 5 na kuwajeruhi 15.Bomu jingine lililotegwa kwenye gari,liliripuka nje ya kituo cha petroli katika mji wa Hillah ambako Washia wengi huishi.Na kaskazini mwa nchi si chini ya raia 2 waliuawa na 11 walijeruhiwa baada ya bomu kuripuka kwenye uwanja ulio katikati ya mji wa Kirkuk.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com