BAGHDAD: Mapigano makali yazuka Diwaniyah | Habari za Ulimwengu | DW | 26.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Mapigano makali yazuka Diwaniyah

Mapigano makali yamezuka katika mji wa katikati mwa Irak, Diwaniyah, hii leo kati ya wanamgambo wa kishaia na maafisa wa polisi kufuatia shambulio dhidi ya kikosi cha jeshi la Irak.

Mapambano hayo yameanza wakati watu waliokuwa wamejihami na bunduki walipokishambulia kikosi hicho cha jeshi la Irak katika eneo la kaskazini la mji huo wa Washia.

Msemaji wa polisi mjini humo amesema mapigano bado yanaendelea na motokaa mbili za polisi zimechomwa moto na magari ya kubeba wagonjwa hayawezi kuingia katika eneo la mapigano kuwaokoa majeruhi.

Sambamba na hayo, wanajeshi wa Marekani waliowasili kusini mashariki mwa Baghdad wameanza kuziharibu boti zilizo kwenye mto Tigris na mitandao inayoingiza mabomu ya kutegwa kando ya barabara mjini Baghdad.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com