BAGHDAD : Maliki atetea serikali yake kuinusuru Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 10.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD : Maliki atetea serikali yake kuinusuru Iraq

Waziri Mkuu wa Iraq Nuri al Maliki amesema serikali yake imeweza kuzuwiya Iraq isitumbukie kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe na ameahidi kujizatiti katika kuleta usuluhishi nchini humo kati ya Washia walio wengi na Masunni walio wachache.

Akitetea kuongezwa kwa wanajeshi wa Marekani nchini humo Maliki ameliambia bunge kwamba umwagaji damu katika mji mkuu wa nchi hiyo umepunguwa kwa asilimia 75.Kiongozi huyo wa Iraq amelihutubia bunge masaa machache kabla ya Kamanda wa Marekani nchini Iraq Generali David Petraeus kutowa ushahidi mbele ya bunge la Marekani juu ya mkakati wa Rais George W. Bush wa Marekani kuongeza wanajeshi wake nchini Iraq.

Balozi wa Marekani nchini Iraq Ryan Crocket pia anakabiliwa na masuali kwenye bunge la Marekani. Ushahidi wao unahesabiwa kuwa muhimu katika kuamuwa vita hivyo vinapaswa kuendeshwa vipi katika kipindi cha usoni nchini Iraq.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com