AUBURN HILLS : DaimlerChrysler kukupunguza ajira 3,000 | Habari za Ulimwengu | DW | 15.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

AUBURN HILLS : DaimlerChrysler kukupunguza ajira 3,000

Kampuni ya magari ya Ujerumani na Marekani ya DaimlerChyrsler imetangaza mipango ya kupunguza ajira za watu 3,000 katika kampuni yake tanzu ya Chyrsler huko Marekani yenye kuleta hasara.

Kampuni hiyo ya magari imesema katika taarifa kwamba pia itafunga mojawapo ya kiwanda chake cha Marekani katika juhudi za kuziba hasara ya kampuni yake hiyo ambayo imekula hasara ya euro bilioni 1.1 mwaka jana.

Dieter Zetsche mwenyekiti wa kampuni hiyo Zetsche ameuambia mkutano wa waandishi wa habari huko Auburn Hills Michigan nchini Marekani kwamba hafuti uwezekano wa kuuzwa kwa kampuni hiyo tanzu hatua ambayo washika dau nchini Ujerumani wamekuwa wakiitetea.

Mauzo makubwa ya kampuni hiyo ya magari aina ya Mercedes yameiwezesha kampuni hiyo ya DaimlerChrysler kurekodi faida katika mwaka 2006 iliofikia jumla ya euro bilioni 5.5.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com