Aubameyang mchezaji bora wa Bundesliga 2016 | Michezo | DW | 03.02.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Aubameyang mchezaji bora wa Bundesliga 2016

Pierre-Emerick Aubameyang amewapiku wachezaji wengine waliowika mwaka jana kushika nafasi ya kwanza kama mchezaji bora wa ligi ya Bundesliga.

Bundesliga |  1. FC Köln - Borussia Dortmund (picture-alliance/dpa/F. Gambarini)

Pierre-Emerick Aubameyang

Na mshindi ni..........Pierre-Emerick Aubameyang!

Mashabiki wa DW wamemchagua mshambuliaji matata wa Borussia Dortmund na mchezaji wa timu ya taifa ya Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang, kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya kandanda ya Ujerumani, Bundesliga, mwaka 2016. Aubameyang alimshinda kwa kura chache mshambuliaji wa Bayern Munich, Robert Lewandowski.

Aubameyang, aliyeuanza mwaka huu wa 2017 kwa kuichezea timu yake ya taifa ya Gabon katika mashindano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika nyumbani, alifunga mabao 23 katika Bundesliga kwa klabu yake ya Borussia Dortmund mwaka uliopita, yakiwamo 16 aliyoyatia wavuni tangu kuanza kwa msimu huu wa 54 wa Bundesliga.

Mbinu zake za kuufumania wavu na kasi yake vimeleta mabadiliko makubwa kwa Dortmund katika miezi 12 iliyopita. Aubameyang, mwenye umri wa miaka 27, pia anawavutia mashabiki nje ya uwanja kwa mtindo wake wa nywele, aina ya nguo anazovaa na jinsi anavyopenda magari ya kifahari.

Mshambuliaji huyo wa Dortmund ameng'ara sana dhidi ya wachezaji wengine wakali, hususan Robert Lewandowski, ambaye alishika nafasi ya pili kwa ufungaji magoli msimu uliopita. Nafasi ya tatu katika shindalo la DW ilishikwa na Joshua Kimmich wa Bayern Munich.

Matokeo kamili ni kama ifuatavyo:

Pierre-Emerick Aubameyang 34.4%

Robert Lewandowski 32.8%

Joshua Kimmich 8.5%

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com