Aubameyang akaribia kujiunga na Arsenal | Michezo | DW | 29.01.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Aubameyang akaribia kujiunga na Arsenal

Kabla ya mchuano wa Jumamosi, suali lilikuwa ni je, atajumuishwa kikosini au la? Peter Stoeger akalijibu kwa kumweka katika kikosi cha kwanza kwa ajili ya kuongoa mashambulizi ya Borussian Dortmund dhidi ya SC Freiburg

 Lakini Pierre Emerick Aubameyang hakuwa na wakati mzuri katika uwanja wa nyumbani wa Signal Iduna Park. Alifurukuta uwanjani bila kufanya chochote na alizomewa na mashabiki wa timu yake.

Sasa ripoti za Ujerumanin na Uingereza zinasema kuwa uhamisho wake wa kwenda Arsenal unakaribia. Gazeti la Ujerumani la KICKER limeripoti kuwa Arsenal na Dortmund wamekubaliana bei ya euro milioni 63 kwa ajili ya uhamisho wa Mgabon huyo mwenye umri wa miaka 28…na kama sehemu ya makubaliano hayo, mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud huenda akahamia Ujerumani kwa mkopo hadi mwishoni mwa msimu. Lakini ripoti hiyo imesema Giroud bado anatafakari kuhusu mkataba huo maana angependelea kubakia England huku Chelsea ikionekana kumuwinda. Kwa mujibu wa Shirika la utangazaji la Uingereza BBC, Dortmund ilikataa kitita cha euro milioni 50 kutoka kwa Arsenal wiki iliyopita.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Yusuf Saumu