ASMARA : Eritrea yajitowa IGAD | Habari za Ulimwengu | DW | 22.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ASMARA : Eritrea yajitowa IGAD

Eritrea imesema leo hii kwamba imesitisha uwanachama wake katika jumuiya ya maendeleo kanda ya Afrika Mashariki baada ya mvutano na hasimu wake mkubwa Ethiopia juu ya suala la Somalia mwezi huu kutishia kuligawa eneo hilo.

Kujitowa huko katika Mamlaka ya Maendelo ya Kiserikali IGAD ni ishara ya karibuni kabisa ya kudhoofika kwa uhusiano kati ya serikali ya Eritrea na nchi za eneo hilo kutokana na mzozo wa Somalia ambapo mamia ya watu wameuwawa katika mapigano wiki hii.

Katika taarifa kwenye tovuti ya serikali Eritrea imesema imelazimika kuchukuwa hatua hiyo kutokana na ukweli wa kurudiwa kupitishwa kwa maazimio kadhaa yasiowajibika ambayo yanadhoofisha amani na usalama wa eneo hilo kwa kutumia kisingizio cha IGAD.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com